Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba mambo bado magumu Ligi ya Mabingwa, yaambulia sare ugenini

IMG 6567.jpeg Mchezo wa Simba dhidi ya Asec Mimosas umemalizika kwa sare ya bila kufungana

Sat, 24 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Simba SC imetoa sare ya bila mabao na wenyeji, ASEC Mimosas usiku wa Ijumaa katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mbingwa Afrika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny Jijini Abidjan, Ivory Coast.

Kwa matokeo hayo, Simba SC inayofundishwa na Kocha Mualgeria, Abdelhak Benchika inafikisha pointi sita na inabaki nafasi ya pili, nyuma ya ASEC Mimosas yenye pointi 11 baada ya wote kucheza mechi tano.

Jwaneng Galaxy ya Botswana yenye pointi nne inashika nafasi ya tatu na Wydad Athletic ya Morocco yenye pointi tatu inashika mkia baada ya wote kucheza mechi nne kuelekea mechi baina yao Jumamosi Botswana.

Mechi za mwisho ni Simba na Jwaneng Galaxy Jijini Dar es Salaam na Wydad dhidi ya ASEC Jijini Casablanca.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: