Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba hawakupaswa kumwacha Kanoute

Kanoute Msdz Simba hawakupaswa kumwacha Kanoute

Wed, 10 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Boiboi Mkali amesema kuwa aliyekuwa kiungo mkabaji wa Simba Sc, Sadio Kanoute hakupaswa kuondolewa kwenye kikosi cha timu hiyo.

Kanoute ambaye ni raia wa Mali, ameondoka Simba SC baada ya kumalizika kwa mkataba wake ndani ya Wanalunyasi.

"Kanoute alipaswa kuendelea kuwepo Simba kwa misimu mingine zaidi yaani sio Kwa msimu huu unaokuja tu hata misimu ijayo walipaswa Kanoute wambakishe,ni ngumu sana kumtengeneza Kanoute mwengine, mchezaji ambae ana uwezo pia wakukupa magoli.

"Sijajua kwanini Simba wameamua kumuacha Kanoute ila kama wamemuacha kwa kuwategemea hawa wachezaji wanaowasajili tusije tukadanganyana na hizi clip za mitandaoni zinazopostiwa. Kanoute alipaswa aendelee kubaki ndani ya kikosi cha Simba," amesema Boiboi Mkali.

Sadio Kanoute analengwa kipaumbele na Klabu ya JS Kabylie ya nchini Algeria ambayo inanolewa na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha.

Benchika tayari amefanya mawasiliano na Kanoute kujua hali yake haswa na kama angependa kucheza Algeria. Aliondoka Simba SC baada ya kumalizika kwa mkataba wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: