Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga zaruhusiwa usajili mpya robo fainali CAFCL

Simba Yanga WA0007 Simba, Yanga zaruhusiwa usajili mpya robo fainali CAFCL

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limefungua usajili kwa timu ambazo zimefuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika ili kufanya mabadiliko kwenye vikosi vyao.

Wachezaji wapya wanaweza kuongezwa kwenye orodha iliyopo kuchukua nafasi ya wachezaji walioondoka kwenye klabu kwenda kuzitumikia timu zao za Taifa wakati huu wa michezo ya FIFA Series 2024 inayoendelea katika nchi mbalimbali.

Michezo ya robo fainali itaanza wikiendi hii ambapo kwa Tanzania Simba itamenyana na Al Ahly ya Misri (Machi 29) huku Yanga ikimenyana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini (Machi 30).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: