Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Tunakwenda kuweka heshim kwa Raja Casablanca

Baleke Simba H.jpeg Simba: Tunakwenda kuweka heshim kwa Raja Casablanca

Wed, 22 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imesema mchezo wao wa mwisho wa makundi ya Kombe la Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca utakaopigwa Machi 31, 2023 nchini Morocco utakuwa mchezo wa kuweka heshima kwa Mnayama.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Kitengo cha Habari wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally kuelekea mchezo huo huku timu zote mbili zikiwa zimeshafuzu kuelekea hatua inayofuata ya robo fainali.

"Mchezo wetu na Raja una umuhimu ni mchezo ambao tunahitaji kuweka heshima, Wametufunga mechi ya kwanza haitokuwa vyema kwa simba kufungwa mara mbili na klabu moja"

"Ukienda kwa kujilegeza Raja Casablanca anaweza kukutia aibu akakufunga goli nyingi. Lazima tuingie kwenye mchezo huo kwa umakini wa hali ya juu ili kuepuka aibu ambayo inaweza kutukumba," amesema Ahemd.

Simba ainakwenda Morocco ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa na Raja katika mchezo wao wa kwanza kwa bao 3-0 kwenye Dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: