Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Tunachotaka kwa Namungo ni ushindi tu

Cadena 2 768x512 Kocha Daniel Cadena.

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daniel Cadena, Kaimu Kocha Mkuu wa Simba amesema wamefanya maandalizi mazuri kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru, leo Novemba 9, 2023. Ikumbukwe kwamba Simba imetoka kushuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Yànga, Novemba 5 2023.

Cadena ambaye aliwahi kuinoa Azam FC kwa upande wa makipa alianza kazi kwenye upande huo akiwanoa Aishi Manula, Ally Salim ndani ya kikosi cha Simba kwa sasa amepewa timu nzima kwa muda.

Kocha huyo amesema: “Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Namungo tunaamini utakuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa lakini tutapambana.

“Wachezaji wapo tayari na wanatambua kwamba tunachohitaji ni matokeo, mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuwa pamoja nasi kuongeza morali kwa wachezaji,”.

Ni Novemba 9 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: