Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC kimewakuta nini?

Simba Simba Simba.jpeg Simba SC

Wed, 21 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mpira wa miguu ni mchezo wa wazi kila mwenye ufahamu anaona kwa macho na kizuri na kibaya kitaonekana.

Msimu uliopita klabu ya Simba ilionekana inawachezaji wazee na waliokuwa Vijana walionekana wamechoka na mwisho wa fagio likapita.

Lakini tuangalie wachezaji wa kigeni Simba SC waliopitiwa na fagio msimu huu;

1. Freddy Michael: Simba SC to USM Alger

2. Sadio Kanoute: Simba SC to Js Kabylie

3. Babakar: Simba SC to Js Kabylie

4. Henock Inonga: Simba SC to As Far Rabat

5. Moses Phiri: Simba SC to ZESCO

6. Clatous Chota Chama: Simba SC to Young Africans SC

7. Louis Miqusson: Simba SC to UD Songo

8. Aubin Kramo

9. Willy Essomba Onana: Simba SC to Al Hilal

11. Saido Ntibazonkiza

12: Pa Omar Jobe.

Nashawishika kuamini huenda shida ilikuwa sio wachezaji bali viongozi walishindwa kuwaunganisha kwa kujua au kutojua.

Hii inatafsiri nyingi lakini kwa upande wangu napenda niwe na hii hapa, Simba SC haikuwa mbaya uwanjani kuna kila dalili shida ikawa kwa uongozi kushindwa Kumanage (Utawala) na kuwaunganisha wachezaji.

Ukiangalia hakuna mchezaji aliyeenda timu ya kijinga! Inawezekanaje mchezaji aonekane bora na Wydad au USM Alger halafu sisi tuseme ni mbovu au ameshuka kiwango?

Tusipokuwa makini hata hawa waliyopo tunaweza kuwavuruga pia. Lakini mbona wanabadilishwa wachezaji ila viongozi ambao tunaamini mawazo yao yamegota mwisho hawabadilishwi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: