Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC: Wiki ya "Thank You" inakaribia

Ahmed Ally Wiki Ya Thank You Ahmed Ally, Ofisa Habari wa Simba SC

Sat, 1 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Mashabiki wakiwa wanaendelea kujiuliza maswali juu ya nini uongozi umepanga kurudisha makali ya kupambana na Yanga ambao wamewatangaza Ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya tatu mfululizo.

Meneja wa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally ameandika;

“Kila kitu muda wake ukifika tutaweka hadharani, kwa sasa tunamshukuru Kocha Mgunda na Selemani Matola na benchi zima la ufundi, wamefanya kazi kubwa sana kuifanya Simba kumaliza katika nafasi hiyo. Wachezaji wote wa Simba wamepambana lakini haikuwa riziki na kumaliza nafasi hiyo ya tatu.”

“Taarifa rasmi, mipango yote ya Simba tutaanza kuiweka rasmi baada ya ligi kumalizika, Tuiache wiki hii ipite lakini kuanzia wiki ijayo tutaanza rasmi kuachia taarifa rasmi nani tunamuondoa,”

“Simba tumemaliza ligi vibaya, mtasikia taarifa nyingi sana huyu anaondoka huyu anakuja lakini tutulie. Maamuzi ambayo tutayafanya yatakuwa sahihi kwa maslahi ya Simba,”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: