Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC Mpya inakuja, Mpanzu aikataa AS Vita

Mpanzu Elie Mpanzu.

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba inaendelea kusuka upya kikosi chake na sasa imeonyesha jeuri ya pesa katika kuwania saini ya winga wa kulia Elie Mpanzu (22), kutoka AS Vita ya DR Congo.

Ikumbukwe kwamba hapo awali tuliripoti kwamba Elie Mpanzu yupo kwenye mazungumzo na Simba na tayari kila kitu kilikuwa kinaenda sawa.

RAIS wa Klabu ya AS Vita, Amadou Diaby alikutana na winga Elie Mpanzu Kibisawala ili kumshawishi aendelee kubaki ndani ya timu hiyo baada ya kuhusishwa kuhitajika na Mnyama.

Uhakika wa taarifa hiyo upo wazi ni kwamba Simba imeshamalizana na mchezaji huyo, na muda wowote wanaweza kumtambulisha kwenye familia yake mpya ya Soka.

Taarifa kutoka DR Congo zinaeleza kwamba, Mpanzu ameshawaaga wachezaji wa timu hiyo huku akiwaambia anataka kupata changamoto sehemu nyingine jambo ambalo limemfanya Amadou kufanya kikao cha siri na mchezaji huyo.

Katika kikao hicho inaelezwa hawajafikia muafaka wa kile anachotaka mchezaji huyo, huku ofa aliyowekewa na timu yake ikiwa ni kubwa kuliko ya Simba japo mchezaji mwenyewe ameonyesha utayari wa kuondoka ili kutafuta changamoto sehemu nyingine nje ya mji wa Kinshasa.

Taarifa tulizozipata zinaeleza kwamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba ambaye kwa sasa ni mjumbe baada ya kujiuzulu nafasi hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ alifika DR Congo kufanikisha usajili wa Elie Mpanzu ambao ulikuwa unataka kupeperuka.

“Ni kweli Try Again yupo Congo, lakini siwezi kusema kwamba ameenda kwa ajili ya dili hilo kwa sababu huwa ni mtu ambaye anaenda nchi mbalimbali kwa mambo yake binafsi. Kama ni hivyo sawa ila siwezi kukuhakikishia,” kimesema chanzo kutoka ndani ya Simba.

Simba wanafanya sajili kimyakimya, na wanaacha wachezaji ambao wamejiridhisha hawana msaada tena na timu, akiwemo Clatous Chama ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Yanga. Huku pia ikiwa imeshawapa mkono wa kwaheri wachezaji kadhaa akiwemo Saidoo Ntibazonkiza, Chilunda, Kennedy Juma, Bocco.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: