Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Day, Kwa Mkapa yageuka gulio

Mkapa Gulio Simba Day, Kwa Mkapa yageuka gulio

Sat, 3 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Simba hawana jambo dogo, achana na nyomi la watu waliokuwa wanaingia uwanjani kushuhudia timu hiyo ikiadhimisha kilele cha siku ya Simba Day lakini uwanjani hapo ni kama pamegeuka gulio.

Leo Simba inaadhimisha Tamasha la Simba Day ambayo imepewa jina la Ubaya Ubwela ikiambatana na burudani ya mechi ya kirafiki kati ya Simba na APR ya Rwanda itakayopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 1:00 usiku.

Nje ya uwanja huo kwa sasa ni kama umegeuka gulio kwa kuuza kila aina ya bidhaa kuanzia vyakula, maji na jezi mpya.

Pembezoni kidogo ya uwanja huo wakina mama wauza vyakula wameweka miamvuli wakiuza chakula kama wali wapo wauza ndizi na vinywaji vya kila aina.

Kwa sasa ukitaka kila aina ya bidhaa unaikuta uwanjani hapo wale wa kuuza makava ya simu, chupa za maji ambazo zimepambwa na nakshi ya rangi nyekundu na wauza pombe.

Wauza jezi nao wapo kila karibu ya eneo wakiuza, lakini zikitawala zaidi nyekundu na nyeupe huku wengine wakichanganya na njano na kijano za Yanga.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: