Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki Simba: Refa ametubeba, tungepigwa nane jana

Pacome Debora Shabiki Simba: Refa ametubeba, tungepigwa nane jana

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nabii Meja amesema hayo jana baada ya timu yake ya Simba SC kufungwa kwa mara ya tatu mfululizo na Yanga, kipigo cha bao 1-0 kwenye nusu fainali ya Ngao ya Jamii, mchezo uliopigwa katika Dimba la Mkapa.

“Kiukweli refa angechezesha mpira jana kwa haki, Simba tulikuwa tunakufa goli nane. Refa alikuwa anaua mashambulizi ya Yanga, lakini Simba walicheza faulo nyingi sana na hakuwaadhibu lakini faulo za Yanga aliziona, kiukweli refa alishindwa kumudu pambano.

“Mashabiki wa Yanga na viongozi wao hawajalalamika sana ni kwa sababu walipata ushindi lakini endapo angetangulia Simba kupata bao pengine mchezo ungekuwa wa vurugu sana. Hata kama hiyo penati ya Kijili tungepewa, halafu matukio yote angeenda nayo vizuri, tulikuwa tunakufa.

“Kiukweli jana tulikuwa tunacheza hovyo na tulikuwa tunakimbia kimbia tu, hakuna mpira wowote tuliocheza pale. Huyu kocha wa Simba hana muda mrefu pale, kati ya makocha wenye uwezo mdogo waliokuja Simba ni pamoja na huyu Fadlu.

“katika wachezaji ambao jana walituadhibu ni huyo Fernandes Debora, aligawa mipira mingi sana hatari kwa Yanga, lakini Yanga nao hawakuwa hatari sana jana lakini wangeamua kufanya ukatiri wangetupiga bao nyingi mno.

“SGR (Joshua Mutale) alikuwa anacheza utoto mwingi, anakokota mipira umbali mrefu na timu yote imepanda juu, akipokonywa tunashambuliwa. Fernandes alikuwa anacheza na jukwaa ashangiliwe, kiukweli jana tulicheza hovyo,” amesema Nabii Meja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: