Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki Simba: Mangungu amejitakia mwenyewe

Mangungu Try Again(1) Shabiki Simba: Mangungu amejitakia mwenyewe

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki maarufu wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome amesema kuwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Murtaza Mangungu ameingia kwenye mgogoro na mashabiki wa timu hiyo kwa kujitakia mwenyewe kutokana na kauli zake.

Mchome amesema hayo baada ya Simba kuwa na matokeo mabovu ambapo katika mechi tatu za mwisho kuanzia kipigo cha bao 5-1 kutoka kwa watani zao Yanga, sare ya bao 1-1 na Namungo na sare ya bao 1-1 na ASEC Mimosas ya nchini Ivory Coast katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

"Mangungu ameingia kwenye matatizo kwa kujitakia, wakati mashabiki wanalalamika timu haichezi vizuri, yeye alitoka kwenye vyombo vya habari akasema kikubwa alama tatu, kama umeshindwa kushabikia Simba tafuta michezo mingine ukashabikie.

"Baadae akasema wanaoshinikiza watu kufanya haya tunawajua na dawa yao iko jikoni. Zile kauli timu ikija kufanya vibaya watu wana-deal na wewe. Try Again yeye sio mtu wa vikao, alisema Rais wa FIFA alimwambia timu zinazocheza hapa haziifikii Simba, yeye akajitoa kijanja.

"Mangungu ameingia kwenye matatizo kwa kuyataka mwenyewe, kwa hiyo amalizane na mashabiki. Wanatakiwa watoke hadharani wasema sio kutumia wachezaji. Wamemtumia Kibu Denis kusafisha hali ya hewa, ameoga matusi kama elfu tatu wakati ndio mchezaji tunayemtegemea.

"Uongozi utoke wenyewe, Mangungu, Try Again, Ahmed Ally waitishe press wazungumze tatizo linalotusibu simba ni nini," amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: