Klabu ya Barcelona ‘La Blaugrana’ imemteua mkongwe Sergi Roberto kuwa nahodha mpya wa timu hiyo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania amekuwa Barcelona tangu ajiunge na shule ya soka mwaka 2006.
Anarithi unahodha kutoka kwa Sergio Busquets aliyeondoka klabu hiyo hivi karibuni kuungana na mchezaji mwenzake wa zamani Lionel Messi katika timu ya Inter Miami ya Marekani.
Sergi Roberto mwenye umri wa miaka 31 alijiunga na shule ya kukuza vipaji La Masia ya Barcelona akiwa na umri wa miaka 14 na tangu wakati huo amecheza karibu michezo 350 katika timu ya wakubwa.
Barcelona imetangaza uteuzi wa nahodha huyo kupitia mitandao ya kijamii. Roberto amekuwa nahodha msaidizi wa Busquets kwa muda mrefu.
Akiwa na La Blaugrana, ameshinda Laliga mara saba, Cpa del Reymara sita, Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili na Kombe la Dunia la Klabu la FIFA mara moja.