Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal Yafuzu Kibabe mbele ya Malawi

Senegal And Guinea Advance In The African Cup Senegal Yafuzu Kibabe mbele ya Malawi

Wed, 19 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kumaliza namba mbili wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2019, Senegal imemaliza hatua ya makundi katika Kundi B ikiwa imefunga goli moja pekee na kumaliza kileleni mwa msimamo wa Kundi hilo.

Imepata sare tasa na Malawi katika mchezo mwingine ambao wameshindwa kuonyesha kiwango kizuri kwenye hatua hiyo ya mwanzo tofauti na msimu uliopita wa mashindano kama hayo.

Habib Diallo na Sadio Mane walikuwa kwenye nafasi ya mabao kwa Senegal lakini haikutokea hata hivyo Malawi walikosa bahati baada ya penati yao kupingwa na VAR kunako dakika ya 74 ya mchezo.

Malawi wanamaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Kundi B wakiwa na alama nne, Senegal wanaweza kucheza na timu inayoshika nafasi ya tatu kwenye Kundi A, C au kundi D katika hatua ya 16 bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: