Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sadio Mane na Dias hali zao shwari

DC6FD75D 5760 472F B60F 17A938BEDE82 660x400.jpeg Sadio Mane pamoja na golikipa wa Cape Verde Josimar Dias

Tue, 25 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa Senegal Sadio Mane pamoja na golikipa wa Cape Verde Josimar Dias wote wanaendelea vizuri baada ya kukimbizwa hospitali kufuatia tukio la kugongana vichwa wakati wa mchezo wa 16 bora wa AFCON 2021 uliyomalizika kwa Senegal kushinda 2-0.

Josimar alioneshwa kadi nyekundu baada ya tukio hilo kutokea dakika ya 57, Mane aliendelea kucheza hadi dakika ya 63 akafunga goli ila dakika ya 70 akashindwa kuendelea na kukimbizwa hospitali.

Baada ya ushindi huo sasa Senegal wanafuzu kucheza hatua ya robo fainali ya AFCON 2021 na mshindi wa mchezo wa 16 bora wa Mali dhidi ya Equatorial Guinea ndio atacheza nae hatua ya robo fainali ya AFCON 2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: