Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sadio Kanoute amfuata Benchikha JS Kabylie

Kanoutee WA0005 Sadio Kanoute amfuata Benchikha JS Kabylie

Sat, 13 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa kiungo wa Simba Sc, Sadio Kanoute ‘Putin’ ameungana na aliyekuwa kocha wa Wekundu hao wa Msimbazi Abdelhak Benchikha kunako klabu ya JS Kabylie ya Algeria kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na Simba kutamatika.

Inaelezwa kuwa Benchikha ambaye alifanya kazi na Putin wakiwa Msimbazi ndiye aliyetoa pendekezo la kiungo huyo wa kimataifa wa Mali asajiliwe katika timu hiyo.

Kanoute alisajiliwa na Simba msimu wa 2021/22 pamoja na wachezaji wengine akiwemo Pape Sakho, Duncan Nyoni, Nelson Okwa, Mohammed Outtara lakini wote hao walitemwa Msimbazi huku Kanoute akiendelea kusalia kabla ya kuondoka baada ya mkataba wake kutamatika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: