Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho awachimba mkwara Mamelodi

Roberto Oliveira, Robertinho Kwa Robertinho

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameweka wazi kuwa, wako tayari kukutana na timu yoyote hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika bila ya kujali ubora wao.

Tayari timu nane zimefuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambapo leo Jumatano itachezeshwa droo ya hatua hiyo ambapo Simba inaweza kupangwa kucheza dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Esperance (Tunisia) au Wydad Casablanca (Morocco) ambazo zimeongoza makundi yao.

Timu zigine zilizofuzu robo fainali ni CR Belouizdad (Algeria), JS Kabylie (Algeria), Raja Casablanca (Morocco) na Al Ahly (Misri).

Simba imetinga hatua hiyo baada ya kukamata nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi C ikiwa na pointi tisa wakati vinara wa kundi hilo Raja Casablanca wakiwa na 16.

Akizungumza nasi, Robertinho alisema Simba ni timu kubwa na imekuwa katika nafasi nzuri, hivyo hana cha kuhofia katika hatua ya robo fainali kutokana na aina ya wachezaji alionao.

“Malengo yangu ni kuona Simba inafikia malengo ya kucheza robo na sasa wanafikiria kucheza nusu fainali ya michuano hii, tunahitaji kuzitumia nguvu zetu katika michezo hii mitatu ya ndani kujiandaa na michezo miwili ya robo fainali.

“Simba ni timu kubwa na inacheza michuano mikubwa, kwa sasa tunasubiri droo na tumejipanga kucheza na yeyote tutakayepangwa naye katika hatua ya robo fainali, hatuna ambacho tunapaswa kuhofia,” alisema Robertinho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: