Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi tisa matata za Cristiano Ronaldo Euro 2024

Ronaldo Euro 6 Cristiano Ronaldo

Tue, 25 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Supastaa, Cristiano Ronaldo anashikilia rekodi tisa matata kabisa zinazohusu michuano ya ubingwa wa Ulaya.

Na bila shaka, staa huyo anayefahamika kwa kifupi kama CR7, anaweza kuongeza rekodi nyingine tamu zaidi kwenye fainali za Euro 2024 zinazoendelea kwa sasa huko Ujerumani, ambako anatazamwa kama mmoja wa wachezaji wenye umri mkubwa.

Kwenye mechi iliyopita, ambapo timu yake ya Ureno iliichapa Uturuki 3-0, Ronaldo alikuwa gumzo baada ya kuasisti bao la Bruno Fernandes, alipofanya hivyo wakati yeye mwenyewe alikuwa na uwezo wa kufunga bao hilo.

Ronaldo, kwanza anashikilia rekodi ya mchezaji aliyefunga mabao mengi kwenye fainali za Euro, akifanya hivyo mara 14. Bao lake la kwanza Ronaldo kwenye fainali za Euro alifunga kwa kichwa dhidi ya Ugiriki kwenye Euro 2004.

Staa huyo anashikilia pia rekodi ya kucheza mechi nyingi za Euro, 27, huku pia akiwa ameshiriki kwenye fainali nyingi za mikikimikiki hiyo, ambapo hizi fainali za Euro 2024 ni fainali zake za sita kushiriki, huku kwenye fainali hizo, amefunga kwenye fainali tano na hizi tu ndiyo bado hajatupia nyavuni.

Supastaa huyo anayekipiga Al Nassr, anaongoza pia kwa asisti kwenye fainali za Euro, akifanya hivyo mara nane, huku akishika rekodi pia ya kutengeneza nafasi nyingi za mashambulizi kwenye michuano hiyo ya Ulaya, akifanya hivyo mara 47.

Ndiye mchezaji aliyeshuhudia ushindi mara nyingi kwenye fainali za Euro kuliko mchezaji mwingine yeyote, mara 14, huku akicheza pia mechi nyingi kama nahodha wa timu, akifanya hivyo mara 18 na amehusika pia kwenye mechi nyingi alizofunga mabao, akitupia nyavuni kwenye mechi 10.

Huyo ndiye, supastaa Ronaldo, ambaye ni mshindi mara tano wa Ballon d’Or, ambapo kwenye Euro 2024 anasaka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga bao, akifukuzia kuvunja rekodi ya staa wa Austria, Ivica Vastic, aliyefunga bao akiwa na umri wa miaka 38 na siku 257.

Umri wa Ronaldo kwa sasa ni miaka 39, miezi 4 na siku 20.

Wakati Ronaldo akitamba na kuweka rekodi tamu kwenye mikikimikiki ya fainali za Ulaya, kwenye maisha yake kwa ujumla, kuna mastaa wamefaidi zaidi makali ya staa huyo baada ya kucheza naye mechi nyingi kwenye timu zao za klabu na wengine timu za taifa.

Mchezaji ambaye amecheza mechi nyingi zaidi na Ronaldo ni Pepe, mara 345 akicheza pamoja Real Madrid na Ureno, wakati mchezaji anayefuatia kucheza mechi nyingi na mkali huyo wa Ureno ni Karim Benzema, aliyecheza pamoja mara 342 kwenye kikosi cha Real Madrid, kisha anafuatia Sergio Ramos mara 339, Marcelo mara 332 wote kwenye kikosi cha Real Madrid, huku Raphael Varane amecheza na Ronaldo mara 231 kwenye kikosi cha Real Madrid na Manchester United, wakati kipa Iker Casillas amecheza na Ronaldo mara 228 kwenye kikosi cha Madrid, huku Luka Modric walichapa pamoja kwenye mechi 222.

Wachezaji wanaofuatia kucheza mechi nyingi na Ronaldo ni Rio Ferdinand (221, Man United), John O’Shea (215, Man United), Xabi Alonso (208, Real Madrid), Wayne Rooney (206, Man United, Ryan Giggs (204, Man United), Alvaro Albeloa (201, Real Madrid), Isco (188, Real Madrid), Paul Scholes (183, Man United), Gonzalo Higuain (180, Real Madrid, Juventus), Sami Khedira (174, Real Madrid, Juventus), Toni Kroos (170, Real Madrid), Edwin van der Sar (167, Man United), Angel Di Maria (166, Real Madrid), Dani Carvajal (165, Real Madrid), Gareth Bale (157, Real Madrid), Darren Fletcher (155, Man United), Wes Brown (153, Man United) na Mesut Ozil, aliyecheza naye mechi 149 huko Real Madrid.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: