Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Real Madrid wachezea kichapo nyumbani

Real Madrid Villareal Aa 2027076 Real Madrid wachezea kichapo nyumbani

Sun, 9 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Real Madrid imeendelea kupoteza tumaini la kutetea taji la Ligi Kuu nchini Hispania La Liga kufuatia kuchapwa nyumbani bao 3-2 dhidi ya Villarreal mchezo uliopigwa dimba la Santiago Bernabeu Jumamosi.

Katika mchezo huo, wenyeji Real Madrid walipata uongozi wa mapema kupitia bao la kujifunga la beki Pau Torres kabla ya nyota wa kimataifa wa Nigeria Samuel Chukwueze kusawazisha bao hilo.

Vinicius Jr alifunga bao la uongozi kwa juhudi binafsi kabla ya Jose Luis Moralles kufunga bao ambalo lilikuwa na utata kumfuatia madai ya kuotea kabla ya mapitio ya VAR.

Wakati mpira ukielekea tamati Chukwueze alifunga bao la tatu na kufanya mchezo huo kumalizika na hivyo Madrid wanakuwa nyuma kwa pointi 12 ya vinara FC Barcelona ambao wanamchezo mmoja mkononi.

Matokeo ya ushindi kwa Villarreal yanaifanya kukwea mpaka nafasi ya tano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: