Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Piga ua, usikose hizi mechi za makundi Euro 2024 utajilaumu

Piga Ua Piga ua, usikose hizi mechi za makundi Euro 2024 utajilaumu

Tue, 18 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kumekucha, Euro 2024. Ndani ya mwezi mmoja, nyasi za viwanja vya soka huko Ujerumani zitawaka moto.

Mechi 51 zitapigwa ndani ya siku 31, wakati mataiafa 24 tofauti yatakapopigana vikumbo kuwania ubingwa huo wa Ulaya.

Zaidi ya nusu ya mechi za mikikimikiki hiyo zitakuwa kwenye hatua ya makundi. Makundi sita yenye timu nne kila moja, zitachuana zenyewe kwa zenyewe kwa makundi yao kabla ya kuingia kwenye mchujo wa 16 bora, kisha robo fainali, nusu fainali na hatimaye fainali yenyewe.

Kuanzia kwenye mechi za mahasimu hadi kwenye vipute vilivyosheheni mastaa wa maana, hizo ni mechi bila ya shaka zitakuwa na mvuto wa kuvutia mashabiki wengi kutaka kuzitazama. Baada ya kushuhudia mchezo wa ufunguzi wa Ujerumani na Scotland na kisha kipute cha maana cha Serbia na England na Hispania na Croatia, hizi hapa mechi ambazo hupaswi kuzikosa kwenye hatua hii ya makundi.

1.Uholanzi vs Ufaransa (Kundi D)

Siku: Juni 21, 2024

Uwanja: Red Bull Arena Leipzig

Wachezaji wa kuwatazama: Kylian Mbappe na Denzel Dumfries

Uholanzi itakipiga na Ufaransa kwenye mchezo wa Kundi D, ambao matazamio ya wengi itakuwa ni mechi yenye mabao mengi. Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana, Les Blues ilishinda 2-1 shukrani kwa mabao mawili ya Kylian Mbappe, hivyo sasa Uholanzi ya kocha Ronald Koeman safari hii itaingia uwanjani ikiwa na tahadhali kubwa juu ya fowadi huyo mpya wa Real Madrid. Kwa upande wao Ufaransa, nao wanapaswa kumchunga sana, Denzel Dumfries, ambaye amekuwa tishio kubwa kwenye upande wa kulia. Kwenye mechi za kufuzu, kiungo huyo wa kulia, aliasisti mara tano, ambapo anazidiwa na wachezaji wawili, tu Mbappe na Bruno Fernandes wa Ureno kwenye kuasisti mara nyingi.

-Mechi tano zilizopita

Uholanzi 1-2 Ufaransa

Ufaransa 4-0 Uholanzi

Uholanzi 2-0 Ufaransa

Ufaransa 2-1 Uholanzi

Ufaransa 4-0 Uholanzi

2.Hispania vs Italia (Kundi B)

Siku: Juni 20, 2024

Uwanja: Veltins-Arena

Wachezaji wa kuwatazama: Alvaro Morata na Nicolo Barella

Hispania na Italia mara ya mwisho zilikutana kwenye nusu fainali ya UEFA Nations League 2023, ambapo La Roja iliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Fowadi wa zamani wa Stoke City na Newcastle United, Joselu alitoka benchi na kuingia kufunga bao la ushindi kwenye dakika 88 na kuisaidia timu yake kutinga fainali ya michuano hiyo na kwenda kukipiga na Croatia. Zilikutana pia kwenye nusu fainali ya Euro 2020, ambapo safari hii kikosi cha Azzurri ndicho kilichoibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti. Kwenye mchezo huo, Nicolo Barella ndiye mchezaji wa kuchungwa kwa upande wa Italia, wakati Hispania itakuwa na huduma ya Alvaro Morata, ambaye amekuwa tishio.

-Mechi tano zilizopita

Hispania 2-1 Italia

Italia 1-2 Hispania

Italia 1-1 Hispania

Hispania 3-0 Italia

Italia 1-1 Hispania

3.Uswisi vs Ujerumani (Kundi A)

Siku: Juni 23, 2024

Uwanja: Deutsche Bank Park

Wachezaji wa kuwatazama: Granit Xhaka na Toni Kroos

Wenyeji Ujerumani watakipiga na Uswisi kwenye mechi yao ya mwisho ya Kundi A, ambayo bila shaka inaweza kuwa ya maamuzi. Miamba hiyo mara ya mwisho ilikutana Oktoba 2020 kwenye Nations League, ambapo mechi hiyo ilizalisha mabao sita, sare ya 3-3. Shughuli itarudi tena safari hii wakitarajia kukutana kwenye Euro 2024. Na kazi kubwa itakuwa kwenye sehemu ya kati ya uwanja, vita ya viungo baina ya nahodha wa Uswisi, Granit Xhaka na shujaa wa Ujerumani, Toni Kroos. Viungo hao wawili wote wamekuwa kwenye viwango bora kabisa, ambapo Xhaka aliipa Bayer Leverkusen ubingwa wa Bundesliga bila ya kupoteza, wakati Kroos alinyakua taji lake la sita la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa Real Madrid.

-Mechi tano zilizopita

Ujerumani 3-3 Uswisi

Uswisi 1-1 Ujerumani

Uswisi 5-3 Ujerumani

Uswisi 0-4 Ujerumani

Ujerumani 3-1 Uswisi

4.Uturuki vs Ureno (Kundi F)

Siku: Juni 22, 2024

Uwanja: Signal Iduna Park

Wachezaji wa kuwatazama: Kenan Yildiz na Cristiano Ronaldo

Uturuki itakipiga na Ureno kwenye mechi ya pili ya Kundi F na hakika mechi hiyo ina mambo mengi yanayovutia kuitazama. Kikosi cha kocha Roberto Martinez ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kubwa ya kushinda michuano hiyo, wakiongozwa na supastaa wao Cristiano Ronaldo, ambaye alimaliza akishika namba mbili kwa mabao kwenye mechi za kufuzu Euro 2024, alipofunga mara 10 nyuma ya Romelu Lukaku wa Ubelgiji. Wakati huo, Uturuki yenyewe itakuwa na huduma ya kinda matata kabisa, Kenan Yildiz, ambaye alionyesha kiwango bora sana alipokuwa na Juventus kwenye Serie. Mechi hiyo itakuwa na radha ya mshambuliaji mwenye umri mkubwa, Ronaldo na kinda mwenye umri wa miaka 19, Yildiz. Je, nini kitatokea? Utu uzima dawa, au ujana ni maji ya moto? Ngoja tuone.

-Mechi tano zilizopita

Ureno 3-1 Uturuki

Ureno 1-3 Uturuki

Ureno 2-0 Uturuki

Ureno 2-0 Uturuki

Ureno 1-0 Uturuki

5.Croatia vs Italia (Kundi B)

Siku: Juni 24, 2024

Uwanja: Red Bull Arena Leipzig

Croatia vs Italy

Wachezaji wa kuwatazama: Josko Gvardiol na Federico Chiesa

Croatia itakutana na Italia kwenye mechi ya tatu ya Kundi B na hakika matazamio ni kwenda kuona mechi yenye burudani. Timu hizo mbili zinamiliki wachezaji wenye uwezo mkubwa na utamu wa mechi yao utatokana na matokeo ya mechi zao zilizotangulia. Josko Gvardiol, amekuwa kwenye kiwango bora sana huko Manchester City kwenye upande wa kushoto, lakini atakutana na shughuli pevu ya Federico Chiesa. Shughuli itabaki kuwa hivyo, hata kama kocha Zlatko Dalic ataamua kumtumia Gvardiol kwenye nafasi ya beki wa kati. Fowadi Chiesa ndiye aliyebeba matarajio makubwa ya Italia kwenye kufanya vizuri katika fainali hizo za Euro 2024 huko Ujerumani.

-Mechi tano zilizopita

Croatia 1-1 Italia

Italia 1-1 Croatia

Italia 1-1 Croatia

Italia 0-2 Croatia

Italia 1-1 Croatia

6.Denmark vs England (Kundi C)

Siku: Juni 20, 2024

Uwanja: Deutsche Bank Park

Wachezaji wa kuwatazama: Jude Bellingham na Rasmus Hojlund

England itacheza na Denmark iliyofika nusu fainali Euro 2020 na hakika mchezo huo unatazamiwa kuwa na mvuto mkubwa kwenye Kundi C. England iliichapa Denmark 2-1 katika mechi nne bora ya michuano hiyo iliyopita, hivyo kipute hicho cha Frankfurt kinaweza kuwa cha kisasi au cha Three Lions kuendeleza ubabe wao kwa wapinzani hao. Mechi hiyo itakayokuwa ya pili kwenye hatua ya makundi katika kundi hilo, England matumaini yao yatakuwa kwa Jude Bellingham, wakati Denmark yenyewe inaamini straika kinda wa Manchester United, Hojlund kuna kitu anaweza kukifanya katika mchezo huo.

-Mechi tano zilizopita

England 2-1 Denmark

England 0-1 Denmark

Denmark 0-0 England

England 1-0 Denmark

Denmark 1-2 England.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: