Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nje kwa Mkapa ni misosi na pamba

Mashabiki Simba SC SC Nje kwa Mkapa ni misosi na pamba

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati mashabiki wakiwa nje ya Uwanja wa Benjamin Mkapa ni mwendo wa biashara ambapo waliojiongeza kwa kuuza vyakula, vinywaji na jezi wameendelea kupiga fedha.

Makundi makubwa ya mashabiki yameendelea kufika hapa ambapo wakati wakijipanga kuingia uwanjani wamekuwa wakijipatia huduma hizo kabla ya kuanza kuingia kwenye foleni.

Mama ntilie na hata sehemu za starehe zinazouza vinywaji na chakula zimekuwa na wateja wengi ambao ni wale waliokuja kwa ajili ya mchezo wa Simba dhidi ya Al Ahly saa 12:00 jioni.

Kwenye maeneo hayo ya starehe kumekuwa na muziki ukiwaburudisha mashabiki hao ambao wapo wanaocheza na kusikiliza huku wakiendelea na huduma.

Mbali na huduma hizo za vyakula na vinywaji pia wapo wafanyabishara wa vifaa vya michezo hususan jezi na vitu vingine vya ushangiliaji nao wanajipigia pesa.

Mashabiki wamekuwa wananunua jezi hizo kwa wingi zikiwa zimewekwa kwenye mahema tofauti tofauti nje upande wa pili wa barabara ya kuingia Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: