Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngoma, Mzamiru wajipange

Debora Fernandez Mavambo 2Qd.jpeg Debora Fernandes Mavumbo

Wed, 10 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna kazi kubwa kwenye safu ya viungo wakabaji wa Simba SC, hasa kwa nyota Mzamiru Yassin na Fabrice Ngoma kutokana na usajili mpya wa kiungo, Debora Fernandes ndani ya klabu hiyo.

Simba imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji huyo kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea klabu ya Mutondo Stars ya Zambia.

Usajili wa Debora unaenda kuwapa wakati mgumu viungo waliopo ndani ya kikosi hicho , Mzamiru, Ngoma na Sadio Kanoute.

Akizungumza nasi, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema Debora anamudu kucheza kiungo mkabaji (namba sita) ingawa anafurahi kucheza namba nane.

Amesema ujio wa kiungo huyo unaongeza nguvu katika eneo hilo, anauwezo wa kuzuia na kupiga pasi sahihi kuelekea mbele na kuanzisha mashambulizi.

“Tunaendelea kusuka timu imara kwa ajili ya muda mrefu maana ya usajili wetu umezingatia umri wa wachezaji wanaosajiliwa, kwa kuongeza mtu katika kila idara na kuifanya Simba bora,” amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: