Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndoto ya Hans Pope kwa Awesu kucheza Simba yatimia

Hans Pope X Awesu Ndoto ya Hans Pope kwa Awesu kucheza Simba yatimia

Wed, 17 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji, Awesu Awesu ndoto ya kucheza Simba imetimia leo Julai 17, 2024 baada ya kutambulishwa Msimbazi kwa kandarasi ya miaka miwili akitokea KMC.

Mwaka 2016 alikaribia kujiunga Simba akitokea Madini FC ya Arusha baada ya kumkosha aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Marehemu Zakaria HansPoppe.

Hans Poppe alionekana akizungumza na kiungo huyo katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha baada ya mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (ASFC), Simba ikiichapa Madini FC bao 1-0 na kutinga nusu fainali ya mashindano hayo.

Akizungumza na wachezaji wa Madini uwanjani hapo, Hanspoppe alisema: “Nawapongeza wachezaji wote na benchi la ufundi maana mmeonesha soka ambalo sikutegemea, lakini zaidi ya yote natoa shukrani za dhati kwa injini yenu huyu kijana rasta (akimwonesha Awesu Awesu) kweli anajua mpira na alitufanya kama alivyotaka.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: