Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nani atavunja hizi rekodi Euro 2024?

Euroooooo Nani atavunja hizi rekodi Euro 2024?

Sat, 15 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati michuano ya Euro ikianza jana kwa mechi ya ufunguzi, moja kati ya mambo yanayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa timu mataifa mbalimbali ni kuona nani ataweka rekodi na nani atavunja rekodi.

Historia inaonyesha kuna rekodi kibao ambazo zimekuwa zikiishi kwa muda mrefu. Hapa tumekubainishia rekodi zote zinazoishi ambazo zinaweza kuvunjwa kwenye fainali za mwaka huu.

MECHI NYINGI ZAIDI KWENYE MICHUANO YA UROPA

Kwa wachezaji wa ndani Ronaldo ndio anaongoza kwa kushiriki michuano hii wakati kwa ujumla anafungana na golikipa wa zamani wa Real Madrid ambapo wote wamecheza fainali tano.

Lakini Ronaldo anaenda kuivunja rekodi hii mwaka huu na kuwa kinara.

MCHEZAJI MWENYE UMRI MKUBWA ZAIDI

Gabor Kiraly anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kushiriki michuano hii aliyoiweka mwaka 2016 akiwa na umri wa miaka 40 na siku 86 alipoichezea Hungary dhidi ya Ubelgiji.

Rekodi ya Kiraly iko hatarini kuvunjwa na beki wa kati wa Ureno, Pepe, ambaye atakuwa na umri wa miaka 41 na siku 113 wakati taifa lake linacheza dhidi ya Jamhuri ya Czech Juni 18 kwenye michuno ya mwaka huu.

MCHEZAJI MWENYE UMRI MKUBWA ZAIDI KUFUNGA BAO

Rekodi hii inashikiliwa na Ivica Vastic kutoka Austria ambaye alifunga bao katika michuano ya mwaka 2008 akiwa na umri wa miaka 38 na siku 257.

Ronaldo anaenda kwenye michuano hii akiwa na miaka 39, hivyo akifunga atakuwa anaivunja rekodi ya staa huyu.

MCHEZAJI MWENYE MABAO MENGI MSIMU MMOJA

Mwaka huu pia huenda ikavunjwa rekodi ya Michel Platini ya kufunga mabao mengi zaidi kwenye kalenda ya shindano moja la Euro, alifanya maajabu haya mwaka 1984 ambapo aliingia kambani mara tisa akiwa na Ufaransa.

Wachezaji kadhaa wanaweza kuvunja rekodi hii ikiwa pamoja na Kylian Mbappe, Harry Kane, Ronaldo na Romelu Lukaku.

MFUNGAJI MKONGWE ZAIDI

Leonardo Bonucci ndiye mfungaji mwenye umri mkubwa zaidi katika fainali ya michuano hii, aliweka rekodi hiyo akiwa na umri wa miaka 34 na siku 71 alipofunga bao dhidi ya England kwenye fainali ya Euro 2020. Rekodi hii huenda ikavunjwa na rekodi katika fainali za mwaka huu.

MCHEZAJI MDOGO ZAIDI

Nyota wa Barcelona Lamine Yamal yuko mbioni kuweka historia yakuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kucheza michuano ya Euro.

Rekodi hiyo kwa sasa inashikiliwa na Kacper Kozłowski, ambaye alikuwa na umri wa miaka 17 na siku 246 alipoiwakilisha Poland kwenye michuano ya Euro 2020, Yamal ataivunja kwa sababu ana 16.

MFUNGAJI WA BAO MWENYE UMRI MDOGO

Mchezaji wa Uswiss, Johan Vonlanthen ndiye anashikilia rekodi yakuwa mfungaji bora mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya mashindano haya. Aliiweka alipofunga bao dhidi ya Ufaransa mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 18 na siku 141.

Rekodi hii itakuwa inawindwa na kinda wa Hispania Yamal ambaye ana umri wa miaka 16 na ameitwa kikosini.

MCHEZAJI MDOGO ZAIDI KUCHEZA FAINALI

Renato Sanches anashikilia rekodi ya mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kucheza fainali, alifanya hivyo mwaka 2016, akiwa na umri wa miaka 18 na siku 327, alipoitumikia Ureno kwenye mechi dhidi ya Ufaransa.

GOLI, HAT-TRICK YA HARAKA

Dmitri Kiritchenko alifunga bao baada ya sekunde 67 tangu kuanza kwa mchezo kati ya Russia na Ugiriki mwaka 2004, pia Platini ndio anashikilia rekodi yakufunga hat-trick ya haraka zaidi, alipokuwa anaitumikia Ufaransa katika mchezo dhidi ya Yugoslavia mwaka 1984 katika hatua ya makundi, akifanya hivyo ndani ya dakika 19 tu.

MABINGWA MARA NYINGI

Ujerumani na Uhispania kwa sasa ndio zinaongoza kwenye sekta hii zikiwa na ushindi mara tatu kila moja na kama moja wapo itashinda basi ndio itakuwa kinara kuliko taifa lolote Ulaya.

Ujerumani ilitwaa ubingwa mwaka wa 1972, 1980 na 1996, huku Uhispania ikishinda 1964, 2008 na 2012, na nchi zote mbili zinatajwa kuwa wapinzani watarajiwa msimu huu wa joto.

MABAO MENGI

Ufaransa inashikilia rekodi yakuwa timu pekee kuwahi kufunga mabao mengi kwenye fainali moja za michuano hii, baada ya kuzifumania nyavu mara 14 mwaka 1984.

Platini alifunga mabao tisa kati ya hayo.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: