Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nacho: Bellingham alizaliwa kuitumikia Madrid

Nacho Bellingham Nacho: Bellingham alizaliwa kuitumikia Madrid

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki na Nahodha wa Real Madrid, José Ignacio Fernández Iglesias ‘Nacho’ amesema Jude Bellingham alizaliwa ili kuichezea The Meringues baada ya kufunga bao lake la sita katika mechi sita alizocheza msimu huu 2023/24.

Bellingham aliifungia Real Madrid bao pekee na la ushindi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Union Berlin katika mchezo wao wa ufunguzi wa Kundi C juzi Jumatano (Septemba 20).

Bellingham aliuwahi mpira uliozagaa ndani ya eneo la yadi sita katika dakika ya 94 huko Santiago Bernabeu baada ya shuti la Federico Valverde kupanguliwa na kufunga bao hilo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England amefunga katika mechi tano kati ya sita alizoicheza Real Madrid hadi sasa.

“Nadhani Jude alizaliwa kuichezea Real Madrid,” nahodha wa klabu hiyo Nacho aliiambia Movistar.

“Tuna bahati kuwa naye hapa pamoja nasi. Tutegemee ataendelea kufunga mabao.”

Goli la Bellingham dhidi ya Union Berlin lilikuwa ni mara yake ya pili kushinda mchezo kwa Madrid katika muda wa nyongeza katika Uwanja wa Bernabeu, baada ya bao lake la ushindi dakika ya 95 dhidi ya Getafe mnamo Septemba 2.

“Tulikuwa na subira,” alisema Bellingham akiiambia Movistar.

“Tulijua tungepata nafasi mwishoni mwa mchezo. Tulilazimika kusonga na mpira, kutafuta nafasi. Tuliendelea, tulionyesha mawazo mazuri na umoja mkubwa.”

Bellingham alifunga mabao 14 kwa Borussia Dortmund katika msimu uliopita, na tayari sasa hivi ameshafunga mabao sita katika msimu wake wa kwanza Bernabeu.

“Ndani ya uwanja nataka kuwa mchezaji, nataka kujaribu kutengeneza vitu kwa wachezaji wenzangu, lakini mpira unapoingia kwenye boksi nataka kuwa muuaji.” alisema.

“Hilo ndilo litakalotushindia michezo. Tunatumahi tutaendelea hivi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: