Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa askari anayekichafua Madrid

Jude Bellingham To Madrid Jude Victor William Bellingham.

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jude Victor William Bellingham alizaliwa Juni 29, 2003 (20) katika Mji wa Stourbridge, West Midlands, England akiwa mtoto wa kwanza wa Mark Bellingham, Sajent wa polisi na straika wa zamani wa mechi za mchangani ‘ndondo’.

Alijiunga na Birmingham City akiwa na miaka minane na amekuwa na timu hiyo tangu wakati huo, mdogo wake Jobe naye yuko kwenye Akademi.

Jude ni mtoto wa kwanza wa Mark Bellingham, ambaye kwa sasa ni Sajenti wa polisi, lakini ujana wake alikuwa straika hatari wa timu za mtaani.

Alisajiliwa na Dortmund mwaka 2020 Kwa ada ya uhamisho ya Euro Million 25 akiwa na miaka 16. Kumbuka Manchester United walishawahi kuhitaji huduma ya Jude mwaka 2019 akiwa na miaka 15 tu lakini kukawa na mvutano Dili Hilo likafa ndipo akasajiliwa Bruno Fernandes.

Baba yake na Jude ambaye ni Polisi ni mzungu pure lakini alimpenda na kumuoa mwanadada aliefahamika kwa jila la Denise raia wa nchini Senegal ambaye ndiye mama mzazi wa vijana wawili Jude Victory William Bellingham na mdogo wake ndiyo maana unamuona Jude ana ka uafrica kidogo ni Senegal Vs England.

Manchester United na Manchester City waliwahi kuhitaji huduma ya Bwana mdogo lakini yeye aliwachagua Real Madrid.

TAKWIMU ZAKE JUDE BELLINGHAM LIGI KUU SPAIN

GAME- 2 GOAL- 3 ASSISTS - 1

Na ndiyo kwanza ana miaka 20 kufikia mwaka huu 2023 lakini anakiwasha namna Ile asipofanta starehe akajituma zaidi Madrid patakua nyumbani kwake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: