Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msimamizi: Kibu ametoroshwa kwenda Ulaya

NonameWE Kibu ametoroshwa kwenda Ulaya

Wed, 24 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimamizi wa Kibu Dennis, Rashid Yazid wa Kampuni ya Football Fraternity amefunguka mapya juu ya sakata la mshambuliaji huyo wa Simba Sc ambapo amesema kuwa nyota huyo ameshawishiwa na ametoroshwa kwenda nje ya Nchi.

“ Kama mlivyoiona taarifa, klabu imekuwa confused kuhusu wapi alipo mchezaji. Siku tatu nyuma nilikosa mawasiliano na mchekeshaji, nikawa na maswali, viongozi wananiuliza yupo wapi mchezaji!” —— Yazid

“Jana tumepata uhakika zaidi kuwa mchezaji yupo Ulaya. Jana ndio ameondoka airport kwenda Ulaya, lakini Mimi nilikuwa najua yeye yupo Kigoma kwa matatizo ya kifamilia.”

“Mchezaji ameshawishiwa na ametoroshwa kwenda Ulaya, mchezaji hana ‘technical know how’ yeye ni mtaalamu wa mpira! ameshawishiwa na kufanya mipango ya kuondoka kwenda Ulaya.”

“Kilichotokea ni utovu wa nidhamu kwanza yeye kwenda Kigoma kwenda kumuuguza mzazi wake hakutoa taarifa kabla baadaye mimi niliitaarifu klabu juu ya suala la matatizo yake ya kifamilia.... Taarifa za kuuguliwa na mzazi alizitoa kwa kiongozi Simba ambaye sio sahihi.”

“Mimi ndiye ninayetambulika na Simba Sc, nimeanza kumsimamia kuanzia dili lake la kwanza Simba Sc, awali nilikuwa mwanasheria ya Kibu tu kabla ya Jamal (aliyekuwa wakala wake) kunikabidhi baada ya kuwa na majukumu mengine nje ya Nchi.” ——Yazid

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: