Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morocco nayo hiyoo yatinga Robo Fainali AFCON

Morocco Celebrate Vs Malawi Morocco yatinga hatua ya Robo Fainali baada ya kuichapa Malawi 2-1

Wed, 26 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya Morocco imefufuzu kucheza hatua ya nane bora kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021 baada ya kuifunga timu ya taifa ya Malawi bao 2-1, ambapo Malawi walikuwa wa kwanza kupata goli mapema kabisa.

Kukiwa na matokeo mengi ya kustaajabisha kwenye Afcon ya msimu huu, Malawi waliiduwaza Morocco yenye mastaa wengi pale ambapo dakika ya saba tu ungwe ya kwanza walipoandikisha goli kupitia kwa Gabadinho Mhango akimalizia mpira mzuri wa John Banda.

Morocco walishtuka na kuanza kusakata kabumbu tulivu kweli wakalipwa na bao la Youssef En-Nesyri kwenye dakika ya 45 kabla ya beki wa Paris St-Germain Achraf Hakimi kufunga goli la ushindi dakika ya 70 ya mchezo huo, kwa shuti kali hatua kama 30 hivi.

Kwa matokeo hayo, Morocco watacheza na mshindi baina ya Misri au Ivory Coast hatua ya robo fainali ya Afcon 2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: