Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morocco, Gabon walee 16 Bora AFCON 2021

Morocco Yafuzu Morocco, Gabon walee 16 Bora AFCON 2021

Wed, 19 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Morocco wametoa sare ya goli 2-2 na Gabon mchezo uliopigwa Jumanne Januari 18, ambapo sasa wamemaliza mechi tatu za hatua ya makundi bila hata kupoteza mchezo mmoja.

Morocco ambao hawajagusa fainali tangia mwaka 2004 ambapo waliishia nafasi ya pili wameongoza kundi C wakiambatana na Gabon kwenye kufuzu kuingia hatua ya 16 bora ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021.

Simba hao wa Milima ya Atlas walitangulia kupata goli kupitia bao la Jim Allevinah kabla ya kusawazisha goli hilo kunako dakika ya Sofiane Boufal.

Gabon walianza tena kupata goli la pili kupitia kwa Nayef Aguerd likiwa ni goli la kujifunga lakini mlinzi wa kulia wa Paris St-Germain Achraf Hakimi kusawazisha kwa faulo.

Morocco wataendelea kubakia katika miji ya Cameroon ambapo hatua ya 16 bora watacheza na timu moja wapo inayomaliza nafasi ya tatu bora kwenye Kundi A, B au C. Gabon watacheza na Burkina Faso Januari 23.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: