Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri yatoa kafara ya kuchinja ili itoboe AFCON 2023

Egypt Misri yatoa kafara ya kuchinja ili itoboe AFCON 2023

Sun, 28 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Soka cha Misri kimefichua kwamba kimechinja ng’ombe kama kafara kwa ajili ya timu yake kufanya vizuri kwenye fainali za Afcon 2023 zinazoendelea huko Ivory Coast.

Msemaji wa chama hicho, Mohamed Morad alisema juzi Ijumaa kwamba ng’ombe amechinjwa na nyama yake imegawawia kwa watu wenye uhitaji huko Cairo ili kuleta bahati kwenye timu hiyo.

Misri bado haijashinda mchezo wowote kwenye fainali za Afcon 2023 na leo Jumapili itakipiga na DR Congo katika mchezo wa hatua ya 16 bora huko San Pedro.

Timu hiyo ilitoka mji wa Abidjan hadi San Pedro kwa ajili ya mchezo huo unaotazamiwa kuwa na upinzani mkali.

Kambi ya timu ya taifa ya Misri imekumbwa na majeruhi wengi. Imempoteza supastaa wake, Mohamed Salah kwa maumivu ya misuli na kipa Mohamed El Shenawy, aliyeumia bega katika mchezo wao wa tatu.

Emam Ashour Jumatano aliwahishwa hospitali baada ya kuumia kichwani mazoezini, lakini sasa amerejea na kujiunga na kikosi hicho kwa ajili ya mikikimikiki hiyo ya hatua ya mtoano.

Wachezaji wa Misri waliripotiwa kutoa kafara ya mnyama mazoezini kwao kabla ya kushinda ubingwa wa Afcon 2008 katika fainali zilizofanyika Ghana.

Na sasa mabingwa hao mara saba wa Afrika, waliotoka sare kwenye mechi zote tatu za hatua ya makundi, watakabiliana na DR Congo, ambayo pia ilitoka sare kwenye mechi zote tatu za makundi, hivyo kila mmoja itahitaji kuandikisha ushindi wake wa kwanza kwa Afcon 2023 usiku wa leo Jumapili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: