Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri, Ivory Coast Mtifuano Mzito Leo

Mohamed Salah Egypt.jpeg Misri, Ivory Coast Mtifuano Mzito Leo

Wed, 26 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

VIGOGO wa Afrika, Misri na Ivory Coast watakuwa dimbani leo katika hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Cameroon.

Timu hizo zina washambuliaji walio katika ubora na kuifanya mechi hii kuwa yenye mvuto zaidi. Mohamed Salah, mshambuliaji wa Liverpool, ataiongoza Misri katika kampeni yao ya kutwaa kombe hilo kwa mara ya 7 katika historia.

Sebastian Haller wa Ajax kwa upande mwingine ni miongoni mwa wachezaji Magiri watakaiongoza Ivory Coast katika kampeni yao ya kuchukua ubingwa huo mara tatu.

Licha ya wachezaji hawa kufunga goli moja moja, lakini wamekuwa wafungaji wazuri katika timu zao za Ulaya. Mo Salah amefunga magoli 54 tangu ulipoanza msimu uliopita wa ligi kuu ya EPL yakiwemo magoli 7 aliyofunga katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Haller wa Ajax ana rekodi nzuri ikiwemo ya kufunga mara 10 katika mechi za mtoano za ligi ya Eufa na anakuwa mchezaji wa pili kufunga katika mechi zote 6 za mtoano akifuatiwa na Cristiano Ronaldo.

Kwa rekodi hizi na nyingine lukuki, mechi hiyo imekuwa na mvuto wa kipekee. Salah ataiongoza Misri ikiwa ni mara ya tatu kuichezea katika michuano hiyo, huku Haller ikiwa ni mara yake ya kwanza.

Licha ya vifo vilivyotokea Jumatatu katika mji wa Yaounde nje ya uwanja , bado mashabiki wanaonekana wana shauku ya kuuona mchezo huu utakaopigwa katika mji wa kibiashara wa Douala.

Misri, licha ya kupoteza kwa Nigeria 1-0 katika mechi ya ufunguzi, inaonekana kupania zaidi baada ya kuwafunga Guinea Bissau na Sudan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: