Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda afichua siri usajili Simba

Mgunda Na Usajili Mgunda afichua siri usajili Simba

Fri, 12 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Aliyekuwa kaimu kocha mkuu wa Simba, Juma Mgunda amefichua siri za usajili mpya wa klabu hiyo iliyopo kambini Ismailia, Misri na kuupongeza uongozi wa timu hiyo kwa kufuata ushauri alioutoa wa kutaka kuvunjwa kwa timu hiyo ili isajili wachezaji vijana ambao watajenga timu mpya.

Mgunda aliiwezesha Simba kumaliza katika nafasi ya tatu ndani ya Ligi Kuu Bara iliyoisha nyuma ya Yanga na Azam akiiongoza katika mechi tisa akishinda saba na sare mbili akimpokea Abdelhak Benchikha aliyetimka kutokana na sababu za kifamilia siku chache baada ya Simba kuchapwa mabao 2-1 na Yanga katika Dabi ya Kariakoo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mgunda alisema hajashangazwa na Simba kufumua kikosi chote kwa sababu ni yeye aliyetoa pendekezo hilo wakati akiwa kocha wa muda wa timu hiyo akitaka timu inaundwe upya kwa kusajili vijana kitu kilichotekelezwa japo sasa yuko nje ya klabu hiyo.

“Simba ilikuwa na wachezaji wengi wenye umri mkubwa na wamehudumu kwa muda mrefu kikosini, walikuwa wanafanya kazi kwa mazoea hilo, nililiona na nilizungumza na viongozi kuwa ili waweze kufanya vizuri wanatakiwa kufanya uamuzi mgumu,” alisema Mgunda, nyota wa zamani wa CDA na Coastal Union.

“Uamuzi wenyewe ni huo walioufanya kwa kuamua kuachana na baadhi ya wachezaji ambao wamedumu kikosini hapo kwa muda mrefu na wenye umri mkubwa na kusajili vijana,” aliongeza kocha huyo msaidizi wa timu ya taifa, Taifa Stars.

Mgunda alisema kuanza upya sio vibaya na walichokifanya Simba ni kizuri na itategemea na usajili walioufanya kama ni bora utawapa matokeo ya kujenga kikosi imara cha ushindani.

“Nilipoachiwa timu niliwaamini vijana na wakafanya kazi nzuri, sio mbaya kuwa na wazoefu lakini ukiwa na damu changa watapambana kuhakikisha wanafanya vizuri ili waendelee kuaminika,” alisema Mgunda na kuongeza;

“Ladack Chasambi, Edwin Balua, Saleh Karabaka ni vijana ambao walikuwa wanatamani kupata nafasi walipopata walionyesha na kuipa matokeo timu hivyo ndio inavyotakiwa wakongwe wanatakiwa kubaki wachache ili kuwapa uzoefu vijana.”

Mgunda alisema anaiona Simba ikijengwa kwa ubora na itaweza kufikia malengo bila kujali ni msimu gani wataonyesha ushindani lakini kitendo cha usajili wa damu changa chini ya makocha vijana kitaifanya timu hiyo kuwa tishio.

“Uvumilivu na kuwaamini vijana kunahitajika, hawapaswi kuwapa presha ya kufanya vizuri ndani ya msimu mmoja, wawaamini na kuwapa muda wa kuzoeana ili waweze kujenga timu bora kama ilivyokuwa kwa watani wao Yanga walikuwa na uvumilivu zaidi ya misimu mitatu hadi sasa wamejipata.”

Wachezaji wapya waliosajiliwa na umri wao kwenye mabao ni; Valentin Nouma (24), Abdulrazack Hamza (23), Joshua Mutale (22), Augustine Okajepha (20), Debora Mavambo (24), Jean Charles Ahoua (22), Yusuf Kagoma (28), Valentino Mashaka (18), Omary Omary (18) na Karabour Chamou (24).

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: