Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu muamuzi wa kwanza mwanamke kuchezesha AFCON

Refaaa Salima Mukansanga, anakuwa mwamuzi wa kwanza mwanamke katika mashindano ya AFCON

Sun, 9 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanawake wakiwezeshwa wanaweza, Salima Mukansanga anakuwa mwamuzi wa kwanza mwanamke kusimama kati na kuchezesha mashindano ya AFCON.

Mwamuzi huyu kutoka Rwanda ataweka historia kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika kama mwanamke wa kwanza kuwahi kuwa mwamuzi wa kati kwenye michuano hiyo mikubwa Barani Afrika.

Salima anakuwa miongoni mwa waamuzi wanne wa kike watakaosimamia mashindano hayo wakiwemo kutoka Cameroon Carine Atemzabong, Fatiha Jermoumi wa Morocco na Bouchra Karboubi ingawa wao hawatachezesha mechi.

Salima ni mzoefu na tayari amesimamia mechi kadhaa ikiwemo za Kombe la Dunia la Wanawake, Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake na Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya CAF.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: