Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi ataja sababu za kuipotezea Barcelona

Messi Pc Data Messi ataja sababu za kuipotezea Barcelona

Thu, 8 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Lionel Messi kujulikana kuwa atajiunga na Inter Miami ya Ligi Kuu Marekani (MLS) na sio FC Barcelona ya Hispania kama ilivyokuwa inajulikana dhamira yake, Messi ameweka wazi sababu za kufuta maamuzi hayo.

“Kiukweli nilitaka sana kurejea Barcelona na nilikuwa na hiyo ndoto, lakini kwa kilichotokea miaka miwili iliyopita, sikutaka tena kupitia hali kama ile, kuweka maisha yangu rehani kwa mtu, nilitaka kufanya maamuzi mwenyewe kufikiria kuhusu mimi na familia yangu”

“Nilisikia taarifa kuwa LaLiga wameniwashia taa za kijani kurejea lakini ukweli ni kwamba vitu vingi vilikuwa vinakosekana kwa ajili ya kukamilisha kurejea kwangu Barcelona, sikutaka kuwa sababu kwao ya kuuza wachezaji na kuwapunguzia mishahara”

“Pesa haijawai kuwa kitu kwangu hatukuwahi hata kujadili kuhusu mkataba na Barcelona, walituma tu proposal lakini haikuwa ofa rasmi, hatukupatana kuhusu mshahara na haikuwa kuhusu pesa au kwenda mimi kucheza Saudia.

“Nina hakika kuna watu ndani ya Club hawakutaka nirejee Barcelona, nilipokea ofa kutoka vilabu vingine Ulaya lakini sikuzizingatia wazo pekee kwa Ulaya ilikuwa ni kurudi Barcelona, ningependa kuwa karibu tena na Barcelona siku za usoni, nitaishi tena Barcelona na familia yangu hilo nilishaamua , natamani kuja kuisaidia hii club siku moja kwa sababu naipenda,” Credit Fabrizio & Mundodeportivo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: