Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mangungu kiti hakikaliki

Murtaza Mangungu Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu

Sat, 3 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baadhi ya mashabiki wa Simba wamekuwa wakimuandama Mwenyekiti wa klabu hiyo, Murtaza Mangungu lakini jamaa ameupiga mwingi kusimamia mambo kwenye tamasha la Simba Day.

Mangungu amekuwa hatulii uwanjani hapa akipita kila eneo ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawasawa hasa kwa mashabiki wa timu yake kuingia uwanjani.

Huku akigoma kuzungumza na chombo chochote cha habari, Mangungu amekuwa akiwasimamisha mashabiki wa timu hiyo waliokuwa wanapata shida ya kutafuta sehemu sahihi ya wanapotakiwa kukaa uwanjani hapo, kulingana na tiketi zao.

Bosi huyo ambaye amekuwa akiandamwa na mashabiki wa timu hiyo kila linapotokea jambo baya, ameonekana pia akikagua tiketi za mashabiki ambao wamekuwa wakisimama kwa muda mrefu milangoni.

Licha ya juhudi za Mwanaspoti kumtaka kusema chochote kigogo huyo hakuwa tayari kuongea na kuondoka haraka eneo ambalo utamsimamisha.

Wakati bosi huyo akizunguka, wapo baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wakimshtukia na kuanza kumuita kwa jina kisha kuwapungia mkono na kuendelea na mambo anayoyafanya.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: