Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United yashusha vitasa kutoka Bayern

De Ligt Noussair 6655783 Man United yashusha vitasa kutoka Bayern

Wed, 14 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester United imethibitisha kukamilisha uhamisho wa walinzi Noussair Mazraoui (kulia pichani) na Matthijs de Ligt wote kutoka Bayern Munich ya Ujerumani kwa mkataba wa kudumu.

Mazraoui (26) raia wa Morocco ametua kwa ada ya Euro milioni 15 na nyongeza ya milioni 5 baadaye huku de Ligt (25) raia wa Uholanzi akijiunga kwa ada ya Euro milioni 45 na nyongeza ya milioni 5 baadaye.

Mabeki hao ambao wamewahi kucheza chini ya Meneja Eric Ten Hag wakati wakiwa Ajax wanaungana na kocha huyo huku de Ligt akisaini mkataba wa miaka mitano wakati Mazraoui akisaini mkataba wa miaka minne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: