Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haaland azua hofu kisa Arsenal

Pep X Haaland Majanga Haaland azua hofu kisa Arsenal

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Straika, Erling Haaland amewapa hofu mashabiki wa Manchester City baada ya kushindwa kuendelea na mazoezi alipokuwa na kikosi cha timu ya taifa ya Norway.

Straika huyo wa Man City, mwenye umri wa miaka 23, alijiunga na timu yake ya taifa kwa ajili ya mechi za kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Czech na Slovakia.

Fowadi huyo alionekana kuumia mazoezini. Picha zilionyesha, straika huyo mwenye kimo cha futi 6 na inchi 4 akitoka kwenye uwanja wa mazoezi huku akishikilia mguu wake.

Man City itakuwa nyumbani Etihad kucheza na Arsenal katika mchezo muhimu kabisa wa kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya mapumziko ya kupisha Kalenda ya Fifa.

Man City chini ya Pep Guardiola itaingia uwanjani kwenye mechi hiyo ikiwa imezidiwa pointi moja na Arsenal. Hata hivyo, kilichoelezwa na daktari wa Norway kinawaondoa hofu mashabiki wa Man City na kuamua mkali wao huyo atakuwapo hiyo siku ya kuwakabili Arsenal.

Haaland alikosa mechi tisa mwanzoni msimu huu baada ya kuumia mguu. Alirejea uwanjani mwishoni wa Januari na tangu wakati huyo amecheza mechi nane za Ligi Kuu England na kufunga mabao manne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: