Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makali ya Fetty Densa yapo huku

Fetty Densa Makali ya Fetty Densa yapo huku

Sun, 10 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Beki tegemeo wa Simba Queens, Fatuma Issa 'Fetty Densa' amesema juhudi na kupambana ndio siri ya kufanya vizuri kwenye michezo mbalimbali aliyocheza akiwa na timu hiyo tangu ajiunge nayo mwaka 2019.

Beki huyo ambaye pia anamudu kucheza nafasi mbalimbali isipokuwa kipa, amekuwa na kiwango bora tangu anaingia Simba na aliliambia Mwanaspoti, sababu za kufanya vizuri ni juhudi zake za ziada pamoja na kuwasikiliza makocha wanataka nini.

"Hakuna siri nyingine zaidi ya kufanya juhudi na bidii zangu za ziada pamoja na yote kumsikiliza kocha, ndio maana watu wanaona tuko bora muda wote. Naamini msimu huu nitafanya vizuri zaidi na kuisadia timu," alisema Fatuma.

Mechi tisa za mzunguko wa kwanza, safu ya ulinzi ya Simba ambayo ndio inaongoza kwenye msimamo wa ligi na pointi 25, imeruhusu mabao matano huku JKT Queens ambayo iko nafasi ya pili ikiruhusu mabao manne.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: