Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lissu: Taifa Stars wakicheza hivi watarudi kula chipsi Dar

Tundu Lissu Bongo Zozo.jpeg Lissu: Taifa Stars wakicheza hivi watarudi kula chipsi Dar

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema kuwa kwa namna ambavyo Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inavycheza, hakuna matumaini iwapo timu hiyo itatoboa makundi kwenda robo fainali ya AFCON.

Lissu amesema hayo akiwa nchini Ivory Coast baada ya kumalizika kwa mchezo wa jana kati ya Stars na Zambia ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, huku Zambia wakisawadhisha dakika za lala salama licha ya kuwa pungufu uwanjani.

“Kwenye mchezo wa mwisho hatuna chochote cha kupoteza, tunataka ushindi, tukipata alama tatu tutasonga mbele aidha kwa kuwa namba mbili au tatu bora, kwa hiyo bado tumo.

“Lakini hatuwezi kuendesha gari kwa kukanyaga breki, unaendesha gari kwa kukanyaga mafuta, wanahitaji kukanyaga mafuta, sio kukanyaga breki, ukikanyaga breki hauendi mbele.

“Wasicheze mchezo kama wa leo (jana), wakicheza mchezo kama wa leo (jana) watarudi nyumbani kula chipsi na mayai Dar es Salaam,” amesema Lissu.

Katika msimamo wa Kundi F, Tanzania inaburuza mkia ikiwa na alama moja tu na bao moja huku Morocco wakiongoza kundi hilo kwa alama 4 wakati Zambia na Congo wakiwa na alama 2 kila mmoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: