Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Elie Mpanzu pagumu, Simba yahamia kwa nyota Nigeria

Elie Mpanzuuuu.jpeg Elie Mpanzu

Fri, 12 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Uongozi wa Simba umeanza mazungumzo na Sporting Lagos FC ya Nigeria ili kupata saini ya winga wa kikosi hicho, Jonathan Alukwu, ikiwa itashindwa kumpata Elie Mpanzu kutoka AS Vita ya DR Congo.

Alukwu mwenye miaka 21, anaichezea FC Heartland, inaelezwa Simba wanajaribu kumshawishi ili ajiunge nao.

TIMU kadhaa za nchini zimeonyesha nia ya kuhitaji saini ya aliyekuwa mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Abalkassim Suleiman.

Nyota huyo wa zamani wa Ruvu Shooting, amemaliza mkataba na Mtibwa iliyoshuka daraja msimu uliopita, na sasa inaelezwa anawindwa na klabu mbalimbali ikiwemo JKU ya Zanzibar.

TIMU ya Coastal Union iko katika mazungumzo na Bandari ya Kenya ili kupata saini ya beki wa kushoto, Siraj Mohamed ‘Mastermind’.

Beki huyo inaelezwa ni moja ya pendekezo la kocha David Ouma raia wa Kenya aliyewataka mabosi wa timu hiyo kuhakikisha inapata saini yake ili akakiongezee nguvu kwa msimu ujao.

BAADA ya Simba Queens kuachana na winga wa klabu hiyo, Wema Richard, tayari Fountain Gate Princess inatajwa kuhitaji huduma yake.

Mazungumzo ya awali yameanza baina ya mchezaji na Fountain ambayo inaelezwa karibu wachezaji sita muhimu wanaweza kuondoka kutokana tatizo la kifedha.

JKT Queens imeanza mazungumzo na aliyekuwa beki wa kulia wa Simba Queens, Diana Mnally aliyemaliza mkataba wake.

Awali, JKT waliwahi kumuazima beki huyo kwa ajili michuano ya CECAFA ikielezwa baada ya kumaliza mkataba na Simba sasa watamsajili rasmi kama mchezaji wao.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: