Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Nigeria ataka Mastraika kufunga mabao

Nigera 2023 Wachezaji wa Nigeria

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Nigeria, Jose Peseiro amesema kazi ngumu sasa inaanza baada ya kikosi chake cha Super Eagles kukamatia tiketi ya hatua ya 16 bora kwenye fainali za Afcon 2023, baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Guinea-Bissau kwenye Kundi A juzi Jumatatu.

Nigeria sasa itakipiga na timu itakayoshika nafasi ya pili kwenye Kundi C, ambayo inaweza kuwa Guinea la kama watakuwa wamewachapa vinara wa kundi hilo Senegal na mechi yao ilitarajiwa kufanyika usiku wa jana Jumanne.

Cameroon nayo inaweza kusonga mbele kama itakuwa imepata ushindi mkubwa mbele ya Gambia, huku wakiombea Guinea ichapwe na Simba wa Teranga.

Nigeria imevuna pointi saba kutoka kwenye mechi zao tatu, lakini imevuka kwa kufunga mabao matatu tu, kitu ambacho kocha wake anadai wanapaswa kupambana kufunga nyingi kwenye hatua waliyofikia.

“Tupo tayari kukutana na timu yoyote,” alisema Peseiro.

“Sijafurahia kwa asilimia 100 kwa sababu tulistahili kumaliza vinara kwenye kundi. Tulistahili kuwafunga Equatorial Guinea (mechi yao ya kwanza) hapo tungekuwa na pointi tisa.”

Peseiro alisema hatua ya mtoano unachezwa mchezo tofauti kabisa na hatua ya makundi, hivyo makosa hasa ya kushindwa kutumia nafasi wanazotengeneza kufunga mabao, yanaweza kuwagharimu pakubwa.

“Ni upinzani tofauti kabisa unakwenda kuanza. Sehemu muhimu zaidi ya upinzani, hatua ya mtoano. Yatupaswa kuwa makini sana mbele ya goli kwa sababu makosa yoyote yanaweza kuwa pigo kwetu.”

Nigeria ina matumaini makubwa kwa straika wao matata kabisa, Victor Osimhen, wakiamini atawafungia mabao muhimu kwenye hatua hiyo ya mtoano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: