Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Misri: Kufuzu ilikuwa haki yetu

Egypt National Team Kikosi cha Misri

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa timu ya Taifa ya Misri Rui Vitoria, amesema timu yake ilistahili kufuzu hatua ya 16 Bora ya michuano ya Afcon 2023 na sasa kazi anayofanya ni kuhakikisha wanashinda mechi zijazo.

Misri juzi ilifanikiwa kutinga kwa hatua hiyo muhimu baada ya kumaliza kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Cape Verde kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi B.

Misri imefuzu baada ya kufanikiwa kutoka sare michezo yake yote mitatu na kukusanya pointi tatu tu, ikimaliza nafasi ya pili nyuma ya vinara Cape Verde yenye pointi nne.

"Tulistahili kuwa na nafasi yetu kwenye hatua ya 16 bora, tulifanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa tunatimiza lengo hilo.”

Hata hivyo, kocha huyo raia wa Ureno amesema timu yake ilikuwa na tatizo kwenye eneo la ulinzi na sasa wanakwenda kulifanyia kazi mazoezini ili waweze kufanya vizuri huko mbele.

"Tulikuwa na makosa mengi kwenye eneo la ulinzi, lakini wengi wanasahau kuwa tumefunga mabao sita kwenye michezo mitatu, ukweli tunatakiwa kuboresha timu yetu kwenye maeneo yote katika michezo inayokuja."

Sasa Misri ambayo mshambuliaji wake mahiri Mohammed Salah, hatacheza hatua hii kutokana na majeraha, inatarajiwa kupambana na mshindi wa pili wa kundi F ambaye atafahamika leo kati ya Morocco, DR Congo, Tanzania na Zambia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: