Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Ivory Coast Louis afungashiwa virago

Kocha Ivory Coast Kocha wa timu ya taifa la Ivory Coast, Jean Louis Gasset

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa timu ya taifa la Ivory Coast, Jean Louis Gasset, amefutwa kazi kulingana na taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka nchini humo, IFF.Kufutwa kazi kwa kocha huyo kuliwasilishwa katika taarifa rasmi ya IFF kufuatia wenyeji hao Fainali za Mataifa ya Afrika kupoteza kwa aibu mabao 4-0 dhidi ya Equatorial Guinea katika mchezo wa mwisho wa Kundi A .

Kutokana na kipigo hicho kikubwa, Ivory Coast imemaliza hatua ya makundi ikiwa na ushindi mmoja tu ambao ni wa mabao 2-0 ambao waliupata dhidi Guinea-Bissau ikumbukwe kuwa walitandikwa kwa bao 1-0 dhidi ya Nigeria.

"Mkataba wa kocha Jean-Louis Gasset na msaidizi wake Ghislain Printant umesitishwa kutokana na matokeo mabaya," taarifa imeeleza.

Ili Ivory Coast ifuzu kwa hatua ya 16 'kama best looser' kama moja ya timu zilizo nafasi ya tatu bora, inahitaji mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na ushindi wa Morocco dhidi ya Zambia na Afrika Kusini kushinda kwa Tunisia.

Wakati huo huo, Ghana nayo imemfukuza kazi kocha Chris Hughton baada ya kutolewa katika hatua ya makundi katika fainali hizo.

Miamba hao wa soka la Afrika maarufu kama The Black Stars, walimaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kundi B wakiwa na pointi mbili, baada ya sare ya 2-2 dhidi ya Misri na Msimbiji baada ya kufungwa mabao 2-1 na Cape Verde katika mechi yao ya ufunguzi.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: