Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiungo Sarr ni mtu na nusu huko Senegal

Pape Matar Sarr Pape Matar Sarr.

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Pape Matar Sarr amekosha wengi hasa mabosi wa klabu yake ya Tottenham Hotspur baada ya kuonyesha soka la kibabe sana akiitumikia Senegal kwenye fainali za Afcon 2023 dhidi ya Cameroon.

Sarr alicheza kwa dakika 74 kwenye kikosi hicho cha kocha Aliou Cisse kilichoshinda mabao 3-1 dhidi ya Simba Wasioshindika kwenye Kundi C huko Yamoussoukro.

Ushindi wa Senegal dhidi ya Cameroon uliiwezesha mabingwa watetezi wa Afcon 2023 kukamatia tiketi ya kutinga hatua ya 16 bora ya fainali hizo zinazofanyika Ivory Coast.

Sarr alifanya vizuri sana kwa muda wake aliokuwa uwanjani katika mechi hiyo, ambapo aliasisti bao la kwanza. Dakika ya 16, kiungo huyo alipiga mpira kwa kichwa ndani ya boksi kutengeneza bao la kwanza lililofungwa na Ismaila Sarr.

Ukiweka kando asisti ya bao la kwanza, mkali huyo wa Spurs alikuwa na ubora mkubwa uwanjani, akipiga pasi sahihi 26 kati ya 31. Aliokoa hatari mbili, alinasa mipira kwenye njia mara mbili, alizuia shuti moja, alipata faulo moja na hakuna mchezaji aliyekokota mpira mbele yake na kumpita.

Mtandao wa Ufaransa wa 90Min ulimpatia mkali huyo wa Senegal alama 7 ya 10 kutokana na ubora wake uwanjani. TNT Sports ilimpa Sarr alama 7 ya 10. Ismaila Sarr pekee ndiye aliyepata alama nyingi kumzidi, 8 ya 10.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: