Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibu Denis arejea kambini Simba, asubiria rungu la adhabu

Kibu Denis Md Simba Kibu Denis arejea kambini Simba, asubiria rungu la adhabu

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Klabu ya Simba, Kibu Denis Prosper amejiunga rasmi na timu yake ya Simba baada kutoonekana katika maandalizi ya msimu mpya 2024/25 ikielezwa alikwenda kufanya majaribio nchini Norway katika timu ya Kristiansund BK inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema Kibu amemalizana na kocha mpya wa timu hiyo Fadlu Davids na ameshaanza mazoezi na wenzake katika dimba la MO Simba Arena Bunju jijini Dar.

Ahmed amesema, Kibu ni kijana wao na alipotoka na kushindwa kufuata taratibu wakati anataka kuondoka hivyo kwa kuwa ametambua kwamba alikosea na amerejea basi wamemruhusu aanze mazoezi lakini taratibu nyingine dhidi yake zitafuatwa. Amesema, taratibu za adhabu zinafuata hivyo mchezaji atakutana nazo lakini kubwa amerejea kikosini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: