Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kante ameanza kufanya yake Euro 2024

Ng'olo Kante Man Award N’Golo Kante

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wa soka wanaamini N’Golo Kante amerudi kwenye ubora wake baada ya kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi kutokana na kile alichokionyesha uwanjani wakati Ufaransa ilipoichapa Austria 1-0 katika mchezo wao wa kwanza wa Euro 2024 huko Ujerumani.

Kiungo huyo alirejeshwa kwenye kikosi cha Les Bleus na kuanza kwa mara ya kwanza baada ya kukosekana kwa karibu miaka miwili, alicheza kwa kiwango bora kabisa katika ushindi huo wa bao 1-0, ambalo lilitokana na mchezaji wa Austria, Maximilian Wober kujifunga.

Kante, 33, alionekana karibu katika kila eneo ndani ya uwanja, akijaribu kuwalinda mabeki wake, huku akisaidia pia kwenye mashambulizi. Kuna tukio moja kiungo huyo wa zamani wa Chelsea alikaribia kabisa kufunga.

Kante, ambaye kwa sasa anakipiga huko Al-Ittihad baada ya kujiunga bure kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana na usiku huo wa Jumatatu na kuchaguliwa mchezaji bora wa mechi. Na kinachoelezwa ni kwamba endapo kama Kante ataendelea kwa kiwango hicho bora, basi Ufaransa itakuwamo kwenye orodha ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa huo wa Euro 2024 huko Ujerumani.

Na mashabiki sasa wanamini Kante yupo kwenye kiwango bora kabisa, ambapo shabiki wa kwanza aliandika: “Achana na Kante yule, huyu wa sasa ndiye Kante haswa.”

Shabiki mwingine alisema: “Hatukumsikia kwa miaka kadhaa mara ghafla tu ameibuka na yupo kwenye viwango. Don Kante, mchezaji matata.”

Mwingine alisema: “Kiwango hiki cha Kante ni cha juu zaidi.” Shabiki wa nne alisema: “Kante amerudi kuwa bosi kwenye jukwaa kubwa.”

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Kante alisema ni furaha kubwa kurudi kwenye timu yake ya taifa na kuanza kuitumikia tena.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2018, ambapo mechi hiyo ilikuwa ya 56 kwake kuichezea Les Bleus alisema: “Nawashukuru wote, nimefurahi kurudi kuichezea timu hii ni kitu kizuri. Napenda kuwa kwenye timu ya taifa. Nimependa mashabiki walipoanza kuliimba jina langu. Asanteni.”

Kante aliichezea mechi 46 timu yake ya Al-Ittihad ambapo ikiwa ni msimu wake wa kwanza Saudi Arabia, timu yake imemaliza nafasi ya tano kwenye msimamo, pointi 42 nyuma ya mabingwa Al-Hilal. Alipokuwa Chelsea, alifunga mabao 13 katika mechi 269 alizocheza kwa misimu saba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: