Jude Bellingham amekuwa na mwanzo wa kushangaza pale Real Madrid, lakini unajua kuna rekodi amevunja baada ya mechi 10 ukimlinganisha na Cristiano Ronaldo?
Ronaldo ndiye lejendi wa Real Madrid akiitumikia klabu hiyo na kuipa mafanikio makubwa ikiwemo rekodi ya kufunga mabao 450 aliyofunga sambamba na kushinda mataji mengi.
Real Madrid hakushinda taji lolote msimu wa kwanza wa Ronaldo 2009–10 akishinda taji la Copa del Rey kwenye msimu wake wa pili.
Ronaldo hadi anaondoka Santiago Bernabeu mwaka 2018 alishinda mataji 15 yakiwemo mawili ya La Liga na manne ya Uefa Champions League. Bellingham ana safari ndefu kabla ya kuanza kukusanya makombe.
Hapa tunaangalia rekodi ya mechi 10 za kwanza za Bellingham akiwa Real Madrid na kuzilinganisha na zile 10 za kwanza za mwamba Ronaldo alipojiunga na wababe hao wa La Liga msimu wa 2009-10.
MECHI 10 ZA KWANZA ZA JUDE Mechi: 10 Mabao: 10 Assisti: 3 Mapigo huru: 0 Mabao ya penalti: 0 Mashuti: 28 Pasi muhimu: 20 Bao Kwa dakika: 85.7 Dakika bila bao la penalti: 85.7 Bao/asisti kwa dakika: 65.9.
MECHI 10 ZA KWANZA ZA RONALDO Mechi: 10 Mabao: 10 Assists: 1 Mapigo huru: 2 Mabao ya penalti: 1 Mashuti: 59 Pasi muhimu: 21 Wastani wa bao: 69.8 Wastani wa mabao na asisti: 63.45.