Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ivory Coast mabingwa AFCON 2023

Ivory Coast Afcon 2023 Champions Ivory Coast mabingwa AFCON 2023

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Ivory Coast walipoteza mechi mbili kwenye hatua ya makundi na kushinda mechi moja huku wakifuzu hatua ya 16 bora kama ‘best looser’ akiwa na pointi 3.

Waliwasukumiza Mabingwa watetezi, Senegal nje ya michuano kwa ushindi wa penalti 5-4 kabla ya kuwaondosha Mali kwa ushindi wa 2-1 kwenye robo fainali.

Katika hatua ya nusu fainali waliwaondosha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kabla ya kutwaa ndoo kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Nigeria kwenye fainali.

Nahodha Troost-Ekong alianza kuitanguliza Nigeria kwa goli la kichwa dakika ya 38’ kabla ya Frank Kessie kuisawazishia Ivory Coast dakika ya 62 kisha Sebastian Haller kupachika bao la kuongoza dakika ya 81

Kombe limebaki katika ardhi ya Ivory Coast baada ya wenyeji kutoka nyuma 1-0 na kushinda 2-1 dhidi ya Nigeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: