Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ivory Coast Yabanwa na Wabishi Sierra Leone Afcon 2021

Sierra L Sirra Leone walisawazisha goli dakika za lala salama kwa uzembe wa Golikipa wa Ivory Coast

Sun, 16 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sierra Leone wamelazimisha sare ya goli 2-2 na timu ya taifa ya Ivory Coast katika mchezo wa Kombe la Mataifa Bingwa Afrika AFCON 2021 mtanange uliopigwa mjini Douala Leo Jumapili Januari 16.

Ukiwa ni mchezo wa pili hatua ya makundi kwa kundi E, Ivory Coast ikiwa imesheheni majina makubwa kama Wilfred Zaha, Nicolas Pepe, Erick Bailly na Franck Kessie walitangulia kupata goli kabla ya kusawazishwa.

Tembo hao walipata goli kupitia kwa Sebastien Haller ambaye alitumia vyema pasi murua kutoka kwa winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha muda mfupi baada ya Kessie kukosa penati.

Hata hivyo, Sierra Leone walisawazisha goli hilo kupitia kwa Musa Noah Kamara kunako dakika ya 55, winga wa Arsenal Pepe aliipa uongozi tena Ivory Coast kupitia mkwaju wa penati na baadaye dakika za nyongeza Alhadji Kamara kufunga goli la kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 2-2.

Kwenye mechi hiyo mlinda mlango wa Sierra Leone Sangare ameshinda uchezaji bora wa mechi baada ya kuokoa michomo langoni mwake mara nyingi ikiwa ni pamoja na parachichi.

Kwa matokeo hayo, Ivory Coast wanafikisha pointi nne, wakati Leone wanakuwa na alama mbili, Algeria alama tatu baada ya kushinda 4-0 kwa Mauritania.

Mechi za mwisho itakuwa Algeria dhidi ya Ivory Coast na Mauritania dhidi ya Leone siku ya Alhamis.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: