Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inonga aumia Simba ikichezea kichapo

Inonga Simba Kuumia Inonga aumia Simba ikichezea kichapo

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

‘Pira Gwaride’ beki wa kutumainiwa na timu ya Taifa ya DR Congo anayecheza soka la kulipwa Klabu ya Simba Ennock Inonga, jioni ya jana ameumia na kulazimika kutoka uwanjani kwa kubebwa na wenzake.

Inoga aliyeng’ara kwenye michuano ya Afcon iliyotamatika hivi karibuni nchini Ivory Coast akiitumikia timu yake ya taifa aliumia kwenye mchezo wa Ligi kuu kati ya timu yake dhidi ya Maafande wa Tanzania Prinsons ‘Wazee wa Pira Gwaride’.

Mwandishi wa Mtandao huu aliyeketi nyuma ya gori la Simba akikusanya matukio mbali mbali alishuhudia lnonga akigaragara chini wakati Prisons wakifunga bao la Pili lililofungwa na Samson Mbangula na kushangilia kwa Style yao ya Kuku Kishingo’ kama wanavyoonekana pichani.

Inonga alishindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Bakari Hussein. Gemu hiyo iliyotamatika kwa Mnyama Simba kupokea kichapo cha bao 2-1 dhidi wa Wajela jeha hao kutoka jijini Mbeya.

Mwandishi wa habari hizi alitinga kwenye bechi la Simba kujua hali ya lnonga alipofika alishuhudia lnonga akishindwa kutembea lkamradhimu kubebwa na wenzake kuingizwa kwenye vyumba vya Uwanjawa Jamhuri.

Hali hiyo ilizua taharuki kwa baadhi ya mashabiki wa Simba ambao waliamua kushuka jukwaani na kumpa Pole kama wanavyoonekana pichani.

Kwa sasa mashabiki wa Simba wanasubiri ripoti ya madaktari wa Simba juu ya maendeleo ya mchezaji wao huyo kipenzi. Kama kawaida Mtandao huu umekusanya matukio kibao kwenye mchezo huo ambayo yataruka hewani muda si mrefu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: