Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ifahamu miji na viwanja vya Euro 2024

Viwanja Euro Ifahamu miji na viwanja vya Euro 2024

Sat, 15 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mchakamchaka wa kusaka ubingwa wa Ulaya kwenye fainali za Euro 2024 ulianza rasmi usiku wa jana Ijumaa. Kabla ya kufahamu viwanja vitakavyotumika kwenye fainali hizo, kitu muhimu kutambua pia miji, ambayo ina viwanja hivyo, vitakavyoshuhudiwa mastaa wa Ulaya wakionyesha ubabe kwenye kusaka ufalme wa bara hilo wakiwa na timu zao za taifa.

Olympiastadion - Berlin

Berlin umekuwa mji mkuu wa Ujerumani tangu muunganiko uliofanyika 1990. Berlin ni moja ya majiji maarufu huko Ujerumani. Kwenye jiji hilo, uwanja ambao utatumika kwenye fainali hizo za Euro 2024 ni ule wa Olympiastadion Berlin.

Uwezo wa uwanja huo ni kuingiza mashabiki 71,000 na ndio ambao umekuwa ukitumika na klabu ya Hertha Berlin kwa mechi zake za nyumbani.

Mechi kubwa zaidi kuwahi kuchezwa kwenye uwanja huo ni fainali ya Kombe la Dunia 2006 na fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2015. Ndiyo uwanja mkubwa zaidi kwenye fainali za Euro 2024 na umekuwa ukitumika kwa fainali ya Kombe la Ujerumani tangu mwaka 1985.

MECHI ZA HAPA

15/06: Hispania vs Croatia (Saa 1:00 usiku)

21/06: Poland vs Austria (Saa 1:00 usiku)

25/06: Uholanzi vs Austria (Saa 1:00 usiku)

29/06: Raundi ya 16 – 2A vs 2B (Saa 1:00 usiku)

06/07: Robo fainali (Saa 4:00 usiku)

14/07: Fainali (Saa 4:00 usiku)

Cologne Stadium - Cologne

Jiji lenye utajiri wa kihistoria, Cologne ndiko unakopatikana mto wa River Rhine na maskani ya vivutio vingi na ndio mji unaongoza kwa kutembelewa na watalii kwa kuwapo na kanisa kubwa kabisa la Saint Peter na mengine mengi.

Ndani ya jiji hilo kuna uwanja wa soka unaofahamika kwa jina la Cologne stadium, wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 43,000. Ndiyo uwanjani unatumika na timu ya FC Koln kwenye mechi zake za nyumbani. Na mechi kubwa zilizowahi kufanyika kwenye uwanja huo ni fainali ya Europa League mwaka 2020. Uwanja huo ulijengwa kwa ajili ya kutumika kwenye mechi za makundi Kombe la Dunia 2006.

MECHI ZAKE

15/06: Hungary vs Uswisi (Saa 10:00 jioni)

19/06: Scotland vs Uswisi (Saa 4:00 usiku)

22/06: Ubelgiji vs Romania (Saa 4:00 usiku)

25/06: England vs Slovenia (Saa 4:00 usiku)

30/06: Raundi ya 16 – 1B vs 3A/D/E/F (Saa 4:00 usiku)

BVB Stadion - Dortmund

Jiji la Dortmund linatazamwa kama moyo wa utamaduni wa mkoa wa Ruhr. Kipindi hicho eneo hilo lilijipatia umaarufu kwa makaa ya mawe, chuma na bia kwa miaka 50 iliyopita, lakini kwa sasa umebadilika na umekuwa sehemu ya mabadiliko ya kuteknolojia na mambo mengi ya utamaduni na michezo. ikiwamo makumbusho ya soka ya Ujerumani.

Ndani ya jiji hilo ndiko unakopatikana uwanja wa soka wa BVB Stadion, ambao umekuwa ukitumika na timu ya Borussia Dortmund kwenye mechi za nyumbani na una uwezo wa kuingiza mashabiki 62,000. Uwanja huo umekuwa maarufu kwa ushangiliaji wa ‘Ukuta wa Njano” ambao umekuwa ukifanywa na mashabiki wa Dortmund. Umewahi kutumika kwenye mechi nyingi kubwa, moja wao ni fainali ya Kombe la Uefa 2001, iliyokutanisha Liverpool na Deportivo Alaves.

MECHI ZA HAPA

15/06: Italia vs Albania (Saa 4:00 usiku)

18/06: Uturuki vs Georgia (Saa 1:00 usiku)

22/06: Uturuki vs Ureno (Saa 1:00 usiku)

25/06: Ufaransa vs Poland (Saa 1:00 usiku)

29/06: Raundi ya 16 – 1A vs 2C (Saa 4:00 usiku)

10/07: Nusu fainali (Saa 4:00 usiku)

Dusseldorf Arena - Dusseldorf

Jiji la North Rhine-Westphalia, Dusseldorf una wakazi 650,000 na una baa zaidi ya 250 pamoja na migahawa kibao ukiwamo wa Old Town, ambayo inafahamika kama moja ya baa ndefu zaidi duniani. Uwanja huo wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 47,000, ambao umekuwa ukitumika na timu ya Fortuna Dusseldorf kwenye mechi zao za nyumbani. Kwenye mechi kubwa uwanjani huo uliwahi kupotika katika mechi za makundi za Euro 1988. Dusseldorf Arena ni uwanja mdogo kwenye fainali za Euro 2024, lakini bado una uwezo wa kuingiza watazamaji 40,000.

MECHI ZA HAPA

17/06: Austria vs Ufaransa (Saa 4:00 usiku)

21/06: Slovakia vs Ukraine (saa 10:00 jioni)

24/06: Albania vs Hispania (Saa 4:00 usiku)

01/07: Raundi ya 16 – 2D vs 2E (Saa 1:00 usiku)

06/07: Robo fainali (Saa 1:00 usiku)

Frankfurt Arena - Frankfurt

Mji maarufu wa kibiashara, amekaa pembezoni mwa mto Main. Frankfurt ni jiji la tano kwa ukubwa Ujerumani na kutokana na mwenekano wake, umepachikwa jina la ‘Mainhattan’.

Ndani ya jiji hilo ndiko unakopatikana uwanja wa soka wa Frankfurt Arena, ambao umekuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 47,000 na umekuwa ukitumika na timu ya Eintracht Frankfurt kwa mechi zake za nyumbani kwenye Bundesliga na michezo mingine. Uwanja huo ulijengwa mwaka 1925 na umetumika kwenye mechi kubwa kadhaa, ikiwamo Euro 1988 na Kombe la Dunia 2006.

MECHI ZA HAPA

17/06: Ubelgiji vs Slovakia (Saa 1:00 usiku)

20/06: Denmark vs England (Saa 1:00 usiku)

23/06: Uswisi vs Ujerumani (Saa 4:00 usiku)

26/06: Slovakia vs Romania (Saa 1:00 usiku)

01/07: Raundi 16 – 1F vs 3A/B/C (Saa 4:00 usiku)

Arena AufSchalke - Gelsenkirchen

Gelsenkirchen umekuwa maarufu kwa machimbo ya makaa ya mawe na wahunzi wa kihistoria, lakini watembezi wa jiji hilo kwa miaka ya karibuni wamekuwa wakikutana na uoto wa kijani kabisa, kumbi za starehe pamoja na boti za kisasa kabisa.

Ndani ya jiji la Gelsenkirchen ndiko unakopatikana uwanjana wa soka wa Arena AufShalke, wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 50,000 wanaoketi, huku FC Schalke 04 imekuwa ikitumia uwanja huo kwa mechi zao za nyumbani kwenye Bundesliga na michuano mingine. Mechi kubwa zaidi kuwahi kufanyika hapo ni fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2004 na robo fainali ya Kombe la Dunia 2006. Kimsingi, uwanja wenyewe ulizinduliwa 2001.

MECHI ZA HAPA

16/06: Serbia vs England (Saa 4:00 usiku)

20/06: Hispania vs Italia (Saa 4:00 usiku)

26/06: Georgia vs Ureno (Saa 4:00 usiku)

30/06: Raundi ya 16 – 1C vs 3D/E/F (Saa 1:00 usiku)

Volksparkstadion - Hamburg

Jiji la tatu kwa ukubwa huo Ulaya lakini si mji mkuu. Hamburg ni maarufu kwa kuwa na bandari na majumba ya kuvutia kabisa sambamba na utajiri wa historia. Kwenye jiji hilo la Hamburg kunapatikana uwanja wa soka wa Volksparkstadion, wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 49,000 wanaokaa. Uwanja huo ndiyo unaotumika na timu ya Hamburger SV kwenye mechi zao za nyumbani. Mechi kubwa zilizotumika kwenye uwanja huo ni pamoja na fainali ya Europa League 2010 na mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2006. Kwa mara ya kwanza Volksparkstadion Hamburg ulifunguliwa mwaka 1953, lakini ulifanyiwa maboresho 2000 na tulitumika pia kwenye Euro 1988 na Kombe la Dunia 1974.

MECHI ZA HAPA

16/06: Poland vs Uholanzi (Saa 10:00 jioni)

19/06: Croatia vs Albania (Saa 10:00 jioni)

22/06: Georgia vs Czechia (Saa 10:00 jioni)

26/06: Czechia vs Uturuki (Saa 4:00 usiku)

05/07: Robo fainali (Saa 4:00 usiku)

Leipzig Stadium - Leipzig

Ilikuwa maskani ya Johann Sebastian Bach, Leipzig ni mji wa kiutamaduni na historia, ambapo ulitumika kwenye kipindi cha mikutano ya amani waka 1989 katika kuelekea muungano wa Ujerumani.

Kwenye jiji hilo la Leipzig, kunapatikana uwanja wa soka unaofahamika kwa jila hilo hilo la Leipzig, ambao una uwezo wa kuingiza mashabiki 40,000. Klabu ya RB Leipzig imekuwa ikitumia uwanja huo kwa mechi zake za nyumbani kwenye Bundesliga na michuano mingine ya Ulaya. Mechi kubwa zaidi kuwahi kufanyika kwenye uwanja huo ni pamoja na zile za hatua ya makundi kwenye Kombe la Dunia 2006 na kwenye mechi ya hatua ya 16 bora. Uwanja huo wenye paa la kibabe kabisa ulifunguliwa 2004 na umejengwa pembezoni mwa Zentralstadion.

MECHI ZA HAPA

18/06: Ureno vs Czechia (Saa 4:00 usiku)

21/06: Uholanzi vs Ufaransa (Saa 4:00 usiku)

24/06: Croatia vs Italia (Saa 4:00 usiku)

02/07: Raundi ya 16 – 1D vs 2F (Saa 4:00 usiku)

Munich Football Arena - Munich

Munich ni jiji lenye wakazi milioni 1.6. Ndiyo jiji la tatu kwa ukubwa huko Ujerumani, ambalo limekuwa na maeneo mbalimbali yenye kuvutia pamoja na bustani za kutosha za kupiga pombe.

Ndani ya jiji hilo ndiko kunakopatikana uwanja wa soka unaofahamika kama Munich Football Arena wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 66,000. Uwanja huo ndio unaotumika na klabu ya Bayern Munchen, ambapo yenyewe inapocheza hapo, dimba hilo linafahamika kama Allianz Areno.

Mechi kibao kubwa zimepigwa kwenye uwanja huo, ikiwamo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2012 na robo fainali ya EURO 2020. Uwanja huo ulifunguliwa 2005, ulipochezwa na Bayern München na 1860 München. Kinachobadilika kwenye uwanja huo ni rangi tu zinapocheza timu tofauti.

MECHI ZA HAPA

14/06: Ujerumani vs Scotland (Saa 4:00 usiku)

17/06: Romania vs Ukraine (Saa 10:00 jioni)

20/06: Slovenia vs Serbia (Saa 10:00 jioni)

25/06: Denmark vs Serbia (Saa 4:00 usiku)

02/07: Raundi ya 16 – 1E vs 3A/B/C/D (Saa 1:00 usiku)

09/07: Nusu fainali (Saa 4:00 usiku)

Stuttgart Arena - Stuttgart

Stuttgart ni jiji kubwa la viwanja na ni moja ya viwanda maarufu kabisa duniani vya Mercedes na Porsche.

Ni eneo lenye mvuto wa kutosha. Ndani ya jiji hilo ndiko unakopatikjana uwanja wa Stuttgart Arena, wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 51,000 wanaokaa. Ndiyo uwanjani unaotumiwa na timu ya VfB Stuttgart kwenye mechi zake za nyumbani katika mikikimikiki ya Bundesliga na michuano mingine. Uwanja huo uliwahi kutumika kwenye mechi kubwa, ikiwamo ya Kombe la Ulaya 1998 na mechi ya mshindi wa tatu ya Kombe la Dunia 2006. Uwanja huo wa Stuttgart Arena umekuwa ikifanyiwa maboresho mara kadhaa tangu mwaka 1993 na ulitumika kwenye mechi za Kombe la 1974 na 2006 na Euro 1988.

MECHI ZA HAPA

16/06: Slovenia vs Denmark (Saa 1:00 usiku)

19/06: Ujerumani vs Hungary (Saa 1:00 usiku)

23/06: Scotland vs Hungary (Saa 4:00 usiku)

26/06: Ukraine vs Ubelgiji (Saa 1:00 usiku)

05/07: Robo fainali (Saa 1:00 usiku)

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: